Bunge la jumuiya ya Afrika mashariki
huenda likafungwa iwapo baadhi ya viongozi wakuu wa Afrika mashariki
hawataingilia kati kufuatia migogoro ya takriban miezi sita sasa
inayolikumba.
Hali hiyo inatokana na kwamba mataifa yaliowachagua viongozi hao kama wawakilishi wake hayana uwezo wa kuwaadhibu wabunge hao.
Bunge la Tanzania limekiri kwamba halina
uwezo wa kuwasimamisha kazi wawakilishi wake katika bunge hilo, licha ya
kwamba wanaendelea kuzozana.
Hatua hiyo inajiri baada ya chama cha FDC
nchini Uganda kulitaka bunge la nchi hiyo kuwafuta kazi wawakilishi wake
kwa kuwa wabunge hao hawatekelezi wajibu wao.
Bendera za maitaifa wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki.
Bunge la EALA limeshindwa kufanya kazi
katika miezi iliopita huku wanachama wakiwa na mpango wa kumuondoa Spika
wa bunge hilo Maregeret Zziwa kwa madai kwamba ameshindwa kutekeleza
wajibu wake inavyohitajika.
(CHANZO: BBC SWAHILI)
No comments:
Post a Comment