Mkali wao ndani ya Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ akila bata na mtoto mzuri, ‘Zari The Boss Lady’.
Chanzo makini kilicho karibu na Diamond,
kimeeleza kuwa msanii huyo na mama’ke, katikati ya wiki iliyopita,
walikwea ‘pipa’ kwenda nchini humo kwa ajili ya mapumziko mafupi kabla
ya kuhudhuria ‘event’ ya utoaji Tuzo za Channel O (Choamva) ambazo
msanii huyo ameshiriki.
Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Zari wkiwa kwenye picha ya pamoja na Kampani waliyokuwa nayo Sauzi.
Kwenye tuzo hizo, Diamond ameingia katika
vipengele vinne tofauti; Video Bora ya Mwaka, Mwanamuziki Bora
Chipukizi, Mwanamuziki Bora wa Afro Pop na Mwanamuziki Bora wa Afrika
Mashariki.
Chanzo hicho kilisema pamoja na event ya tuzo hizo, Diamond atatumia muda huo kukutana na mtoto mzuri Zari ambaye ndiye anayedaiwa kurithi mikoba ya aliyekuwa mpenzi wake, Wema Sepetu ‘Madam’ waliyemwagana hivi karibuni.
Chanzo hicho kilisema pamoja na event ya tuzo hizo, Diamond atatumia muda huo kukutana na mtoto mzuri Zari ambaye ndiye anayedaiwa kurithi mikoba ya aliyekuwa mpenzi wake, Wema Sepetu ‘Madam’ waliyemwagana hivi karibuni.
Nasibu Abdul ‘Diamond’ akipozi na mama’ke (Sanura Kassim ‘Sandra’).
“Diamond ameona bora aondoke na mama’ke wakale bata lakini pia
watakutana na wifi Zari si unajua tena ndiyo kwanza mahaba niue…project
zinaendelea Sauz,” kilisema chanzo hicho makini.Gazeti hili lilifanya jitihada za kuwasiliana na Diamond ambaye pia aliambatana na dada’ke wa hiyari, Halima Kimwana lakini hakuwa tayari kuzungumzia chochote juu ya ukaribu wake na Zari zaidi ya kuanika picha zilizomuonesha akiponda raha.
No comments:
Post a Comment