Akizungumza baada ya kuulizwa na gazeti hili juu ya mwenendo wa muigizaji Aunt Ezekiel ambaye mara kadhaa huonekana akiwa ‘viwanja’ usiku, daktari mtaalamu wa magonjwa ya kina mama na watoto, aliyejitambulisha kwa jina moja la Dokta Chale, alisema utokaji wa usiku na uvaaji wa viatu virefu unaweza kusababisha matatizo ya nyonga, shida wakati wa kujifungua, miguu kuuma na uvimbe kwenye vifundo vya miguu ‘enka’.
Kuhusu unywaji pombe, Dokta Chale alisema endapo mama mjamzito atafanya tabia hiyo, ipo hatari ya uelewa wa mtoto katika ukuaji wake kuwa mdogo na pia kuchukua tabia zote za mama yake.
...Akizidi kujiachia.
“Viatu virefu na mitoko ya usiku kwa mama mjamzito ina madhara
makubwa sana kwani mtoto atakuwa na uelewa mdogo, yaani akili yake
inakuwa haikui sawasawa, kifupi ana-adapti (kuiga) tabia zote za mama
yake anaweza kuwa zezeta kama mama anatumia pombe,” alisema.Katika kudhihirisha kuwa ustaa ni kazi kubwa, licha ya ujauzito wake kuonekana mkubwa, Aunt Ezekiel amekuwa akijirusha kama kawaida sehemu mbalimbali nyakati za usiku huku wakati mwingine akiwa amevaa viatu virefu.
CHANZO: GPL
No comments:
Post a Comment