EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, December 5, 2014

ESHE BUHETI: NAMVALIA KHANGA MOKO MUME WANGU TU

Katika safu hii wiki hii tunaye mwanadada anayeyaendesha maisha yake kwa kuuza sura kwenye filamu Bongo. Huyu si mwingine bali ni Eshe Buheti.
 
Mkali katika tasnia ya filamu Bongo, Eshe Buheti.
Kama ilivyo ada naye aliwekwa mtukati na mwandishi wetu Imelda Mtema na kuulizwa maswali ambayo alitoa ushirikiano katika kuyajibu.Ijumaa: Unaonekana kutoandamwa na skendo kama inavyokuwa kwa mastaa wengine, hii inatokana na nini?
Eshe: Unajua mimi ni mke wa mtu, najichunga sana kuhakikisha sichafuki kwa namna yoyote, ndiyo maana unaona skendo zinanipitia mbali.

Ijumaa: Hebu tuambie, unapokuwa nyumbani unapendelea kuvaa mavazi gani?
 Eshe: Nikiwa ndani kwangu hasa na mume wangu akiwepo ni mwendo wa khanga moja kwa kwenda mbele.

Ijumaa: Mastaa mbalimbali inakuwa vigumu kuolewa na wakiolewa hawadumu kwenye ndoa zao, wewe unadhani utadumu?
Eshe: Kila jambo anapanga Mungu, kikubwa najitahidi kumheshimu mume wangu na kumfanyia kila linalomfurahisha na kuacha yanayomkera, naamini kwa kufanya hivyo ndoa yetu itadumu.
Ijumaa:  Najua una mtoto mmoja sasa, vipi una mpango wa kuongeza mwingine soon?

Eshe: Mwanangu anaonesha kabisa anataka mdogo wake, kwa hiyo tunajipanga na naamimi hatuna muda mrefu tutafanya maandalizi ya kumleta kiumbe mwingine duniani.
Ijumaa: Wanaume wengi hawapendi kazi ya usanii hasa kutokana na skendo mbalimbali, vipi wewe mume wako amewezaje kukubaliana na kazi yako?
Eshe: Nahisi mume wangu ni mtu wa tofauti, ananiamini na kwa kuwa hajawahi kusikia lolote baya, wala hana wasiwasi.

Ijumaa: Kuna mastaa ambao wana katabia ka’ kuiba waume za watu, siku ukijua kuna anayemnyemelea mumeo utafanyaje?
 Eshe: Huyo atakuwa ananitafuta shari na kwa kweli ajiandae kwa mpambano. Siwezi kuingiliwa kwenye anga zangu halafu nione sawa tu.

Ijumaa:  Kutokana na tabia ya mastaa wengi kuwa na kucha ndefu na kutopenda kiziharibu hata kupika hawawezi, wewe kwako hili likoje?
Eshe: Kwa mambo ya mahanjumati yani hapa ndiyo umefika, omba siku nikualike uje kula kwangu ndiyo utajua mimi ni mpishi au mbabaishaji.

Ijumaa: Ni mambo gani ambayo huyapendi kabisa kwenye maisha yako?
Eshe:  Mimi sipendi umbeya, uvivu, majungu kwani ni vitu ambavyo vinaturudisha nyuma.

Ijumaa: Kwenye sanaa kuna vishawishi vingi sana hasa hii tabia ya baadhi ya maprodyuza kupenda sana rushwa ya ngono, wewe unakabiliana vipi na changamoto hiyo?
 Eshe: Najitambua na ninajiheshimu sana. Siwezi kujivunjia heshima yangu kwa mambo ya kijinga kwa hiyo Mungu ananisaidia navuka changamoto hizo.

Ijumaa: Unawashauri vipi hawa mastaa ambao mabifu ni sehemu ya maisha yao?
Eshe: Hili ni tatizo na kwa kweli ni vyema sisi mastaa tukawa na umoja na tukashirikiana katika kuendeleza sanaa yetu badala ya kugombana.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate