Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Naftari Mlawa ‘Nuhu Mziwanda’ akiwa na bebi wake Zuwena Mohammed ‘Shilole’.
Stori: Waandishi WetuJAMBO limezua jambo, saa chache baada ya mwanadada mtafutaji kunako tasnia ya muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, kuvalishwa pete ya uchumba na mchumba wake, Naftari Mlawa ‘Nuhu Mziwanda’ tayari watu wameanza kuisengenya.
Shilole alivalishwa pete hiyo katika sherehe yake ya kuzaliwa iliyofanyika katika ‘apartment’ za Baraka Plaza, Mikocheni jijini Dar ambapo mara baada ya mwanadada huyo kukata keki na kuwalisha watu mbalimbali waliohudhuria, ndipo Nuhu alipomsapraizi mwanadada Shilole kwa kumvisha pete hiyo.
Kitendo hicho kilionekana kukubalika na waalikwa wengi, lakini wengine hawakufurahishwa nacho kwa madai eti kwamba Nuhu ni mdogo kuliko Shilole hivyo hakustahili kuvisha pete mtu mwenye umri kama dada’ke.
“Mh! Mwenzangu hii kali, mimi siku zote Nuhu niliamini hayupo serious kutembea na Shilole maana ni mkubwa kuliko yeye lakini sasa hapa kanishangaza kweli, kwa nini asitafute mdogo mwenzake?,” alisikika dada mmoja ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake.
Hata hivyo licha ya masengenyo hayo kusambaa chini kwa chini, Nuhu aliwakata watu vilimilimi kwa kutamka hadharani kuwa wanapendana na Shilole hivyo haoni ajabu kama kuna watu hawatakubaliana na penzi lao.
‘Shilole’ akiwa pembeni ya keki yake ya bethidei wakati wa sherehe yake ya kuzaliwa.
“Tukio linalotendeka hapa limepewa baraka zote na wazazi wetu
wameridhia mimi na mchumba wangu tuoane na hii ni hatua ya kwanza tu
mengine yatafuata na msishangae sana kuona wazazi wetu hawapo eneo hili
ni kwamba wanatambua kinachoendelea hapa.“Najua wengi mtakuwa na maswali kuhusu hili, mimi na yeye tunapendana na ndiyo maana leo hii namvisha pete mpenzi wangu na Mungu atatujaalia katika maisha yetu,” alisema Nuhu na sherehe ikaendelea kwa watu kula na kunywa.
Sherehe hiyo ilihudhuriwa na mastaa mbalimbali akiwemo Steven Mengere ‘Steve Nyerere’, Wellu Sengo ‘Matilda’, Shettah, Martin Kadinda, Mh. Temba, Chegge, DJ Choka na DJ Tass.
Steve Nyerere aliyekuwa MC wa shughuli hiyo alisema Shilole ni shemeji yake kwani yeye ni kaka yake Nuhu, na kwamba tukio linalofanyika hapo, wao kama ndugu wamekubaliana na ndoa itafungwa.
“Siku zote huwa namwambia shemeji yangu kuwa yeye ni mtafutaji kwa hatua aliyofikia mpaka sasa na ninamkubalisana shemeji yangu, karibu Iringa,” alisema muongoza sherehe huyo.
Imeandikwa na Shani Ramadhani, Musa Mateja na Gabriel Ng’osha.
No comments:
Post a Comment