EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, January 8, 2015

PANYA ROAD KWISHA KAZI! KOVA ALALA NJE SAA 120


Stori: Haruni Sanchawa na Makongoro Oging’
BAADA ya kuwakosesha amani wakazi wa Jiji la Dar es Salaam usiku wa Ijumaa iliyopita, lile kundi la vijana wahalifu linalojulikana kwa jina la Panya Road limefikia ukingoni baada ya kudhibitiwa kwa kasi kubwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Amani linakupa ‘full stori’.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.
Kundi hilo liliibuka majira ya saa moja jioni ya Ijumaa iliyopita na kufanya vurugu katika maeneo ya Magomeni-Kagera, Dar ikidaiwa kuwa walikuwa wakilipa kisasi baada ya mwenzao aliyefahamika kwa jina la Ayubu Mohamed  ‘Diamond’ kuuawa na wananchi wenye hasira kali.

TUJIUNGE NA KOVA
Akizungumza na wanahabari wetu ofisini kwake jijini Dar juzi, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema tangu siku ya tukio hadi Jumatano (jana) ameendelea na msako maalum wa kuwadaka Panya Road hao ambao ndiyo janga la mjini kwa sasa.
WANAE WAMMISI
“Nimeamua haswa kuwafungia kazi, silali, wanangu wananimisi kwa muda, naingia mzigoni usiku kucha kuhakikisha tunawakamata wahusika wote ambao wanasadikika ni wafuasi wa Panya Road. Hata leo (Jumanne) na kesho (Jumatano) msako upo palepale,” alisema Kova.
ALALA NJE SAA 120
Kutokana na msisitizo huo wa Kova, hesabu za harakaharaka zinaonesha kuwa, tangu Ijumaa iliyopita hadi Jumatano (jana), Kova atakuwa amelala nje kwa siku 5 sawa na saa 120 ambapo muda wa asubuhi anakuwa ofisini kama kawaida, jioni anaendelea na msako  akisimamia vijana wake.

Kundi linalodaiwa ni Panya Road.
WALIOKAMATWA
Kwa mujibu wa Kamanda Kova, hadi juzi Jumanne, idadi ya vijana 510 wanaotuhumiwa kuhusika na kundi hilo walikamatwa sanjari na viongozi wao watatu.
“Ukiachilia mbali wadogowadogo, vinara ambao tumewakamata ni Halfan Nurdini (24), mkazi wa Tandale-Sokoni, Said Mohamed (22), mkazi wa Tandale-Sokoni na Mohamed Ndangula mkazi wa Mburahati jijini Dar,” alisema Kova.
AMA ZAO AMA ZAKE
Akizidi kutilia msisitizo kuhusu kundi hilo ambalo ni maarufu kwa kupora mali za watu katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar, Kova alisema msako unaendelea kwa wale wachache ambao bado hawajatiwa nguvuni basi ama zao ama zake.
“Haiwezekani vijana kama hawa watishie amani, niwaambie tu wale ambao bado hatujawakamata, tutawafikia na wote tutawafikisha kwenye mikono ya sheria,” alisema.
JK APELEKEWA TAARIFA
Imeelezwa kuwa, kutokana na unyeti wa tukio hilo lililotikisa jiji kwa takriban saa nne (Ijumaa), taarifa ya namna ambavyo linashughulikiwa zimepelekwa Ikulu ya Magogoni kwa Rais Jakaya Kikwete ‘JK’ ambapo ametoa maagizo mazito juu ya wahusika.
“JK amepelekewa taarifa, ameelekeza cha kufanyika. Hili tukio halikuwa la kufumbia macho,” kilisema chanzo kilichopo ndani ya jeshi la polisi.
POLISI WAPONGEZWA
Wakizungumza na wanahabari wetu kwa nyakati tofauti, wananchi walilipongeza jeshi la polisi  chini ya Kamanda Kova kwa jinsi walivyolidhibiti kundi hilo.
Abdallah Juma, mkazi wa Tandale alisema kuwa nguvu ya polisi inapaswa kuungwa mkono ikiwa ni pamoja na raia kutoa taarifa zinazohusiana na vikundi kama hivyo.
”Wananchi tunapaswa kuunga mkono jitihada za jeshi la polisi, tukiungana kwa pamoja hakika hakutakuwa na wahalifu mitaani na tutaishi kwa raha mustarehe kuliko siku ile ya Ijumaa usiku,” alisema Abdallah.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
WANASIASA WATAJWA
Chanzo kilicho ndani ya jeshi la polisi kimewaonya baadhi ya wanasiasa ambao wanatajwa kuwashinikiza vijana hao kufanya vurugu katika harakati zao za kisiasa.“Vijana hawahawa wa Panya Road ndiyo wanaotumiwa na baadhi ya wanasiasa katika mipango yao. Huwa wanawapa fedha na kuwatuma kwenda kumzomea mgombea fulani, waache mara moja kwani wanachangia kuwapa nguvu,” kilisema chanzo hicho.
WAJUMBE WA MTAA KUKIONA
Chanzo kingine kimesema kuwa, mkakati umewekwa kuwataka wajumbe wa serikali za mitaa jijini Dar kuhakikisha hakuna Panya Road kwenye maeneo yao na mitaa itakayobainika kuwa na vibaka wengi, wajumbe watawajibishwa.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate