EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, February 3, 2015

HIVI NDIVYO MUME ALIVYOMCHINJA MKEWE HOTELINI


Makongoro Oging’ na Haruni Sanchawa/Uwazi
HUU ni ukatili namba moja kwa wanandoa duniani! Bado picha haijatoka kichwani kwa wakazi wa Manzese jijini Dar kufuatia kifo cha kuchinjwa cha  Josephine Ndengaleo Mushi kinachodaiwa kufanywa na mume wake wa ndoa, Remy Joseph (35).
Remy Joseph (35) anayetuhumiwa kumuua mke wake, Josephine Ndengaleo Mushi.
Tukio hilo la kutisha kusimuliwa achilia mbali kuona, lilijiri saa 9: 10 alasiri ya Januari 29, mwaka huu ndani ya chumba kimoja kilichopo ghorofa ya pili ya  Hotel Friend’s Corner Ltd iliyopo Manzese Argentina, Dar.
KAMA KAWAIDA YA GAZETI LA UWAZ!
Kama kawaida ya Gazeti la Uwazi, kufuatilia matukio makubwa ya kutisha, kusikitisha na hata kufichua maovu. Baada ya habari za mauji hayo kusambaa kama moto wa kifuu, waandishi wetu walianza kuichimba habari hii kwa kina.
SIKU MOJA KABLA YA TUKIO
Kwa mujibu wa mhudumu mmoja wa hoteli hiyo, Januari 28, mwaka huu, Remy na Josephine walifika kwenye hoteli hiyo na kuchukua chumba. Walionekana wenye amani, kwani hakuna sura iliyoonesha kuna tatizo.
“Walikuwa kama wateja wengine. Tena niliwauliza kama wanatoka mkoa, wakasema ni wakazi wa Dar es Salaam, wao ni mke na mume kwa ndoa, waliamua kulala hapa ili kuimarisha mapenzi yao, si lazima kila siku nyumbani,” alisema mhudumu mmoja.

JANUARI 29, SAA 9 ALASIRI, DAMU ZAONEKANA
Kwa mujibu wa baadhi ya wahudumu wa hoteli hiyo, siku ya pili, muda wa saa tisa alasiri, walishtuka kuona damu nyingi ikitoka ndani ya chumba walichopanga wawili hao.“Tulishtuka sana. Tukajua kuna kitu kikubwa kimewapata. Ilibidi tuwagongee mlango ili tujue kilichowapata lakini mlango haukufunguliwa,” alisema mhudumu mwingine.
Mtuhumiwa Remy Joseph akiwa chini ya ulinzi mkali.
POLISI WAITWA
Kwa vile ukimya ulitawala ndani ya chumba hicho huku damu zikiendelea kutiririka, ilibidi uongozi wa hoteli hiyo yenye sifa ya ulinzi, uwasiliane na Kituo cha Polisi cha Ndugumbi ambacho kipo jirani.
Polisi walifika, wakagonga mlango kwa muda mrefu bila kufunguliwa mpaka baadaye sana ambapo mlango huo ulifunguliwa na mwanaume akiwa ameshika kisu mkono wake wa kuume.
POLISI WATUMIA MBINU YA KIVITA
Ndani ya chumba kulionekana damu zimetapakaa kila sehemu. Polisi walimsihi mwanaume huyo kuangusha kisu chini ili waongee lakini jamaa aligoma.
“Polisi walimwamuru mwanaume atupe kisu chini, akakataa. Sura yake wakati huo ilikosa mwonekano wa ubinadamu. Ndipo askari mmoja alitumia mbinu ya kivita, alimpiga mkono wake wa kulia kwa kumshutikiza kisu kikaangukia mbali, akawekwa chini ya ulinzi. Kumbe kile kisu mbali na kumuua mkewe alikitumia kujaribu kujichinja koo lakini ikashindikana,” alisema mhudumu huyo.
MWILI WA MAREHEMU WAKUTWA UMEPIGISHWA MAGOTI
Mwanaume akiwa chini ya ulinzi na pingu mikononi, polisi waliingia chumbani na kukuta damu kila mahali. Cha kusikitisha zaidi, mwili wa marehemu Josephine ulipigishwa magoti, sehemu ya miguu mpaka magoti ikiwa sakafuni na kifuani kulalia kitanda. Halafu ulifunikwa shuka.“Kwa mbali ungeweza kusema kuna binadamu anasali kwa namna ambavyo marehemu huyo alivyokuwa amepigishwa magoti,” alisema mhudumu huyo.
ALITAKA KUJINYONGA
Katika hali iliyoonesha kuwa, mtuhumiwa baada ya kutenda ukatili huo alitaka kujinyonga, polisi walikuta waya wa umeme wa tivii ukining’inia kwenye pangaboi lakini ukiwa umekatika.
Remy Joseph akichukuliwa na Polisi kuchukuliwa hatua za kisheria.
UCHUNGUZI WA POLISI CHUMBANI
Polisi walifanya uchunguzi chumbani na kugundua kuwa, marehemu Josephine alichinjwa shingoni, akakatwa mbavu mbili, moyo na maini vilikuwa nje ‘vikimwagika’, mwisho alichomwa kisu utosini.
LAINI ZA SIMU ZAKUTWA ZIMEKATWAKATWA
Pia kwenye chumba hicho, polisi walikuta simu mbili, ya marehemu na ya mtuhumiwa zikiwa zimeharibiwa laini kiasi cha kukosa mawasiliano.
UWAZI LAZUNGUMZA NA MTUHUMIWA
Uwazi lilipata bahati ya kuzungumza na mtuhumiwa huyo kabla ya kupelekwa Kituo cha Polisi Magomeni, Dar ambapo alisema Josephine alikuwa mke wake na wameishi kwa muda zaidi ya miaka kumi na kupata watoto wawili. Hata hivyo, hakuongea zaidi ya hapo.
UONGOZI WA HOTELI WATOA NENO
Msimamizi mkuu wa hoteli hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Zuberi Hussein alipohojiwa na Uwazi alisema:
“Tuliwapokea hawa watu kama wateja wengine. Walilipa shilingi elfu kumi na tano kwa chumba.  Hatukujua kama haya yangetokea, wahudumu ndiyo walibaini baada ya kuona damu ikitiririka mlangoni.”
MWILI WA MAREHEMU WAPELEKWA MUHIMBILI
Baadaye, polisi waliupakiza mwili wa marehemu kwenye gari kuupeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili huku mtuhumiwa akipelekwa Kituo cha Polisi Magomeni jijini Dar pembeni yake akiwa amelala marehemu mkewe.
WANACHOJUA NDUGU WA MAREHEMU
Baada ya hapo, Uwazi lilifunga safari hadi eneo la Studio, Kinondoni, Dar nyumbani kwa David Ndeshao Mushi ambaye ni kaka wa marehemu na ndiko sehemu ulipowekwa msiba.
Baadhi ya ndugu wa marehemu walidai kwamba, Josephine na mumewe mara kwa mara walikuwa na migogoro  ya ndoa.
“Ndoa yao haikutulia, walikuwa wanapatanishwa lakini baada ya muda mfupi wanaanza tena ugomvi. Mumewe alikuwa akimhisi vibaya mke wake. Hata hivyo, Desemba mwaka jana, Josephine alienda kuishi kwa kaka yake kutokana na ugomvi,”alisema mmoja wa wanandugu wa karibu.
Kaka mtu  huyo alipohojiwa alisema: “Marehemu alirudi kwangu lakini tulikuwa hatujaongea naye kuhusu ugomvi wao. Nilisafiri mkoani nikamuacha, niliporudi, Jumatano alienda kazini lakini hakurudi. Tulipopiga simu yake akawa hapatikani. Mumewe naye akawa hapatikani hadi taarifa ilipotufikia kwamba kauawa hotelini.
“Tunatarajia kusafirisha mwili kwenda Moshi, Jumapili (juzi). Mazishi yatakuwa Jumatatu (jana). Marehemu ameacha watoto wawili ambao walikuwa wakiishi Tabata, Dar.”
MTUHUMIWA, MAREHEMU
Inadaiwa kuwa, mtuhumiwa alikuwa mfanyakazi wa Baa ya Break Point iliyopo jijini Dar. Marehemu alikuwa mfanyakazi katika Kampuni ya TAC iliyopo Upanga, Dar.
Mmoja wa marafiki zake wa karibu alisema Jumatano mchana, mumewe alimfuata kazini na wakawa na mazungumzo, alimtaka waondoke lakini marehemu alikataa.Alimbembeleza sana mwishowe wakakubaliana na kuondoka lakini wakashangaa kusikia alimuua hotelini.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate