EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, February 2, 2015

MBUNGE FILIKUNJOMBE ALAZAMIKA KULALA KATIKA "PAGALE" AKITEKELEZA AHADI YA UMEME KIJIJI CHA KILONDO


Mbunge  wa  jimbo la  Ludewa Deo Filikunjombe akiwahutubia  wananchi wa  kijiji  cha Kilondo Ludewa
a
Mbunge  Filikunjombe  akisisitiza jambo  wakati akizungumza na  wananchi wa kijiji cha Kilondo
Mwenyekiti wa kata ya  Kilondo wa Chadema Bw  Edgar Kyula  akimpongeza  mbunge wa  wa Ludewa  Deo Filikunjombe kushoto  wakati wa mkutano wake  kijijini Kilondo
Baadhi ya  viongozi wa kata ya  Kilondo  wakimpongeza Filikunjombe  kulia
Mbunge  Filikunjombe akikabidhi nyavu za  kuvulia  samaki kwa ajili ya vikundi  vya vijana  wote  Kijiji cha  Kilondo na Lusisi Ludewa
Filikunjombe kushoto akikabidhi vifaa  vya  michezo kwa  vijana  kijiji cha Kilondo ili baada ya kazi kufanya  michezo
Mbunge  Filikunjombe wa tatu  kulia akiwa na viongozi wa kijiji  cha Kilondo na Lusisi ambao aliwapa nyavu na vifaa vya  michezo
Mbunge  Filikunjombe akiwa amembeba mmoja kati ya  watoto  kijiji cha Kilondo  wakati wa mkutano wake kijijini hapo
Kikongwe  mkazi wa kijiji cha Kilondo  akisalimiana na mbunge wa  Ludewa Deo  Filikunjombe baada ya  kumalizika kwa mkutano  wake kijijini hapo
Mtaalam  wa  umeme akimuelekea  mbunge Filikunjombe mambo ya kitaalam baada ya  kutembelea  maporomoko ya mto Makete ambao utatumika kuzalisha  umeme  kushoto ni katibu wa mbunge Filikunjombe Bw Stany Gowele
Mtaalam akimwonyesha maporomoko hayo ya maji mbunge Deo  Filikunjombe
Huu  ndio mto  utakao  zalisha umeme kijiji cha Kilondo Ludewa
Mbunge Filikunjombe akitazama mto huo
Huu ni mto  Makete  unaomwaga maji yake ziwa nyasa
Mbunge  Filikunjombe akitazama mto Makete
Wataalam  wakimwaga maji  yenye  chumvi mto  Makete  ili kupima  nguvu ya maji katika mto huo kwa ajili ya kuanza uzalishaji  wa umeme katika kijiji cha Kilondo Ludewa
Kipimo kwa ajili ya  kujua kasi ya maji katika mto Makete
Wakazi wa kijiji  cha Kilondo Ludewa
Mbunge  Filikunjombe akiongoza  msafara  wake kwenda  kupanda  bodi baada ya  kuamka alfajiri katika kijiji  cha Kilondo Ludewa
Mbunge wa  jimbo la  Ludewa Deo Filikunjombe (kulia) akiwa katika  box huku ameshika tama  eneo la kando ya  ziwa  nyasa juzi alfajiri akisubiri  usafiri wa bodi kuelekea  Matema wilayani Kyela baada ya  kufanya  ziara ya  siku  mloja  kijijini Kilondo  wengine  pichani ni mkurugenzi wa kampuni ya Kilondo Investment  Bw Erick Mwambeleko  wa pili  kushoto ,katibu mwenezi mkoa wa Njombe Honolatus Mgaya na katibu  mwenezi wilaya ya Ludewa Bw  Felix
Msafara  wa mbunge  Filikunjombe ukijiandaa kupanda katika  bodi  Ziwa nyasa
Mwanahabari  Emmanuel Msigwa wa Chanel  Ten akipanda katika bodi
Baadhi ya  wasafiri  wa ziwa nyasa  wakisafiri kutoka Matema Kyela  kwenda Manda Ludewa
Na matukiodaimaBlog
WANANCHI wa  kijiji  cha KIlondo kata ya  Kilondo  wilayani Ludewa mkoani Njombe wamempongeza  mbunge wa  jimbo la  Ludewa Deo Filikunjombe  kwa  kuwa  mbunge  pekee  katika  jimbo  hilo kufika kulala chini ardhini kwenye nyumba isiyo na mlango wala dirisha (Pagale) katika  kijijini hicho toka  nchi ipate uhuru wake mwaka 1961.

Mbunge  Filikunjombe na  msafara  wake  wa watu  zaidi ya 15  walifika katika  kijiji  hicho  cha Kilondo kilichopo mwambao mwa ziwa nyasa  kwa lengo la mbunge  huyo kuwaanzishia  mchakato  wa kupatiwa  umeme  kupitia shirika  lisilo la  kiserikali la Kilondo Investment linalofadhiliwa na mradi  wa usambazaji  vijijini (REA)

Akizungumza kwa niaba ya  wananchi  wa kijiji   hicho mwenyekiti wa  serikali ya  kijiji   hicho Bw Laurian Kyula alisema  kuwa  jimbo  hilo  limepata  kuwa na  wabunge zaidi ya  5 ila   hakuna  mbunge  ambae  alifika na  kukubalia  kulala  katika  kijiji  hicho  kutokana na  kuwa na miundo mbinu mibovu na  kutokuwa na nyumba  ya  kisasa  ya kulala  wageni zaidi ya  nyumba  za  wananchi ambazo  nyingi  zipo kienyeji  zaidi hazina hadhi .

" Kweli tumeshindwa  kuamini  kuona  mbunge anaamua  kulala  kijiji  hapa hata  bila kuwepo kwa maandalizi mazuri ya  kulala ......tumekuwa na  wabunge  wengi  sana ila  wapo  baadhi yao hata kukejeli  kuwa  kijiji   hakina  hadhi ya  kulaza  waheshimiwa  hadi  watakapoboresha mazingira...kati ya  viti ambavyo hatukupata  kufikiria  ni pamoja na kuja  kupokea  mgeni  wa  kiwilaya kuja  kulala  hapa  kijijini ila  wewe  mheshimiwa wetu Filikunjombe umekuwa ni kiongozi wa aina yake" alisema  mwenyekiti   huyo 

Akimpongeza  mbunge  huyo kwa jitihada  zake za  kuwasogezea  huduma  ya  umeme  kijijini hapo  mwenyekiti  huyo    alisema kijiji  hicho   ni moja kati vijiji ambavyo  vipo mwambao  mwa  ziwa nyasa na  uwezekano  wa  kuunganishwa na  umeme  wa gridi ya  Taifa   kutoka  Ludewa mjini ama Kyela mkoani Mbeya ni  vigumu  kutokana na kuzungukwa na milima  na maji hivyo  kwa  upande  wao  waliamini kabisa kamwe hawatakuja  fikiwa na huduma  za umeme.

" Tunashindwa kujua ni  kiasi gani mbunge  wetu  unavyotuhangaikia  kwa mambo ambayo  wengine  waliotangulia  walituhakikishia  kuwa ni  vigumu kufikiwa na huduma ya  umeme kwa  kuwa ni porini labda  hadi tutakaposogea karibu na vijiji  vya nje ya  Mwambao kauli ambazo  vilitufanya  kukata tamaa kabisa kwa  umeme kwetu ni huduma  isiyo wezekana.....ila  tunashangazwa leo kupitia mbunge wetu Jembe Filikunjombe unatuletea wataalam wa kuanza kujenga mradi wa umeme hapa kijijini"
Bw Kyula  alisema kati ya  mambo ambayo  wao  hawata kuja  kusahau  maishani mwao ni utendaji kazi wa mbunge  huyo na  maendeleo makubwa aliyoyafanya katika  jimbo  hilo la  Ludewa kwa kipindi  cha miaka  minne ya  ubunge  wake huku  wapo waliokaa miaka  mitano  bila  kufanya jambo linaloonekana kwa   wananchi  wao.


Hivyo  alisema  iwapo  chama  cha mapinduzi (CCM)  kitataka  kulipoteza  jimbo hilo la Ludewa ni pamoja na  kujaribu  kufanya maamuzi yasiyo hitajika kwa  wananchi yakiwemo ya  kukata  jina la mbunge  wao katika mchakato  wa kuomba  kugombea ubunge    jimbo  hilo la Ludewa na kumpa nafasi  mtu wa kwao watashangazwa na maamuzi magumu ya  wananchi kwa  kulitoa  jimbo hilo upinzani kama  fundisho kwa CCM kupenda wanachopenda  wao na sio wananchi.
Awali  mkurugenzi mtendaji wa  mradi wa Kilondo Investment Bw  Erick Mwambeleko akielezea  mradi huo alisema  kuwa  mpango  wa kuwaunganisha  wanakijiji  hao na umeme  ulikuwepo toka  wakati mbunge Profesa Raphael Mwalyosi akiwa madarakani  ila cha kushangaza kila alipomfuata  kutaka  kusaidia kufanikisha kuanzishwa  kwa mradi huo  aliishia  kutoa kauli za kukatisha tamaa  kuwa haweza  kusaidia  kupeleka  umeme kijijini hapo kwa kuwa ni gizani sana hakuna faida yoyote .

" Ni  kweli kijiji  hiki cha Kilondo  kipo porini  zaidi  ila  kuna  watu  wanaishi hata  mimi Mwambeleko ni mzaliwa wa hapa  hivyo  nimesoma  sayansi na kutumia elimu yangu nikaona  ngoja  nishirikiane na mbunge Filikunjombe  kuleta ukombozi  wa  umeme  huku kwa kupitia  kampuni yangu ya Kilondo Investment kampuni ambayo mchango wa mbunge  ni mkubwa zaidi hadi leo tunaanza mchakato wa kuleta  umeme hapa...."

Alisema  kuwa tayari  fedha kiasi cha  zaidi ya Tsh milioni 300  zimepatikana kwa ajili ya kuanza  utekelezaji wa mradi huo ambapo  fedha  hizo kiasi zimetoka REA na nyingine ni fedha  ambazo ni mchango wa mbunge Filikunjombe .

Pia  alisema  umeme   huo  utazalisha  kijijini hapo  kupitia maporomoko ya maji ya mto Makete  ambayo yanaingia katika  ziwa nysa  na kuwa maporomoko hayo yana nguvu  ya  kuzalisha  umeme KV 50 na  kasi ya maji katika maporomoko hayo ni lita  za ujazo 9312 kwa  sekunde maji ambayo yanatosha kabisa kwa  uzalishaji wa umeme  wa kutosha kaya  zote  kijijini hapo na kijiji cha jirani.
Kwa  upande  wake  mbunge  Filikunjombe akielezea  sababu ya  kulala  kijijini hapo alisema  kuwa moja kati ya ahadi yake kwa  wananchi wa Ludewa ni  kufikisha maendeleo kila  kona ya  jimbo  hilo na kuwa akiwa katika  ziara  pale ambapo  jua litazamia ndipo atakapolala  bila  kujali uwepo wa maandalizi ama lah.
"Wananchi  wote wa Ludewa ni  wapiga kura  wangu hivyo imekuwa ni kawaida  yangu  kuwa nao  wakati  wote na  kulala popote na  kula  chochote ambao  wao  wanakula  siku  zote .....hivyo  jua linapozamia nikiwa  ziarani nitalala hapo bila  kujali maandalizi lengo  kuona  nashirikiana na  wananchi wangu kwa mazingira  yoyote yale......nimefurahi  sana  leo  kulala katika  nyumba  hii inayojengwa ambayo haina sakavu ,milango wala madirisha (Pagale) mimi ni siufanyi ubunge kama ufalme kuwa nikija  mimi ziarani  wananchi wangu  wasumbuke kufanya maandalizi yasiyo ya kawaida"
Kuhusua  mradi  huo wa umeme Filikunjombe alisema  kuwa lengo lake kuona  wananchi hao  wanapatiwa umeme mapema  zaidi  ikiwezekana ndani ya mwaka huu wananchi hao  waweze na  umeme  katika makazi yao  hivyo  kuwaomba  wananchi kutoa  ushirikiano kwa mafundi  waliofika kijijini  hapo kuanza  utekelezaji wa mradi huo pamoja na kuwasaidia  kufanya tathimini ya mahitaji ya taa na ufungaji  umeme katika  nyumba  zao.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate