Prof.
Bakari Lembaliti ambaye ni Mwalimu wa Chuo Kikuu Muhas Muhimbili
akiwapatia miswaki na Dawa watoto wenye ulemavu wa macho baada ya kuwapa
elimu ya matumizi ya usafi wa kinywa na meno inayo endelea kwa siku ya
pili katika Shule ya Msingi Buhangija iliyopo Shinyanga
Prof.
Bakari Lembaliti (kushoto) ambaye ni Mwalimu wa Chuo Kikuu Muhas
Muhimbili akiongea na Mwanafunzi Khassan Shaban ( aliye vaa kofia kulia)
anayesoma katika Sekondari ya Muhumbu Islamic ambaye amedhaminiwa na
Shirika fulani anakwenda na kurudi katika kituo hicho ambapo analipiwa
ada tu na mambo mengine ajitegemea
Mwalimu
wa kitua hicho( aliyeka kulia) ambaye anayehusika naupokeaji wa
watoto hao akiendelea kuwapokea watoto hao wanao letwa na wazazi wao kwa
kuhofia usalama wa watoto wao, leo amepokea zaidi ya watoto 12 toka
sehemu mbalimbali.
Chama
cha Madaktari ,wameendelea kutoa huduma hiyo hata kwa watu wazima
waliofika kufanyiwa usafi wa Kinywa na Meno, mwanadada akiwa amezibwa
meno baada ya kuonekana yametoboka Meno yake.
Raisi
Mstaafu wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno na Daktari Bingwa wa
Watoto Rachel Mhavile toka Hospitali ya Taifa Muhimbili, akifanya
ukaguzi wa kinywa na Meno kwa Kuyela Masuka, aliyeanguka toka juu ya mti
nakusababisha jino lake lambele juu kushotolikawa linaninginia na
kunadaktari aliye jaribu kulirudishia lakini tiba hiyo ikamshinda kwa
sababu hakua amepiga mswaki vuzuri na kumsababishia kupata maambukizi na
kushindwa kufumba mdomo na kutokula chakula, matibabu aliyoyapata toka
kwa Daktari Bingwa huyo ni kung'olewa jino na baadaye watampeleka
Hospitali ya Mkoa kupiga X-rey kuhakikisha Meno ya jirani yaliyotumbukia
kwenye Mifupa hayata athiri.
No comments:
Post a Comment