EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, March 16, 2015

ILIBAKI HIVI TU DIAMOND AKATWE MGUU!


Musa Mateja
Msanii nguli wa muziki wa kizazi kipya na nyota wa Wimbo wa Nitampata wapi aliyewahi kuwa mchumba wa Wema Sepetu, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amenusurika kukatwa mguu katika Hospitali ya TMJ, Mikocheni jijini Dar es Salaam kufuatia ugonjwa wa Foot Corn (maarufu kwa jina la kisahani) kumtesa kwa kipindi kirefu.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, Diamond ambaye kwa sasa anaminya kimalavidavi na mwanamama Zarina Hassan ‘Zari’, alianza kusumbuliwa na ugonjwa huo takribani siku 730 zilizopita (miaka miwili), huku mwenyewe akipuuzia matibabu yake na kuelekeza nguvu kwenye shoo za ndani na nje ya nchi.

Msanii nguli wa muziki wa kizazi kipya na nyota wa Wimbo wa Nitampata, Nasibu Abdul ‘Diamond’.

“Mara kwa mara alikuwa akilalamikia maumivu makali ya mguu lakini kwa kuwa yalikuwa yakija na kupotea, alikuwa akipuuzia kwenda hospitali mpaka juzi (Ijumaa) alipoamua kwenda TMJ,” kilisema chanzo chetu kwa masharti ya kutotajwa jina.

WALICHOKIBAINI MADAKTARI
“Madaktari walipompima, walishangazwa na jinsi alivyokuwa amechelewa kwenda kupata matibabu, nasikia ugonjwa aliokuwa nao ni hatari sana. Kama angeendelea kuchelewa, huenda wangelazimika kumkata mguu kabisa, Diamond aliogopa sana,” kilisema chanzo hicho.
Ikazidi kuelezwa kuwa baada ya vipimo kukamilika na kubainika kuwa alikuwa na Foot Corn, madaktari walimueleza kuwa ni lazima wamfanyie upasuaji wa haraka wa kutoa nyama zilizokuwa zimeota kwenye mguu wake ambazo zilitengeneza kitu kama kisahani.
Staa Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’.
NDANI YA CHUMBA CHA UPASUAJI
Baada ya taratibu zote kukamilika, Diamond aliingizwa ndani ya chumba cha upasuaji ambapo jopo la madaktari kadhaa, wakiwemo wenye asili ya Bara la Asia walimfanyia upasuaji.

SHOO NYINGI ZILISABABISHA ACHELEWE MATIBABU
Kwa mujibu wa chanzo kingine ambacho ni ndugu wa msanii huyo, sababu iliyosababisha Diamond akachelewa kwenda hospitali kutibiwa tatizo hilo, ni kubanwa na shoo nyingi ambapo alikuwa akihofia kwamba akienda hospitali anaweza kulazwa au matibabu yakachukua muda mrefu hivyo kuvuruga mikataba ya shoo ambayo tayarti alikuwa ameshasaini.

MSIKILIZE DIAMOND
Baada ya kukamilika kwa upasuaji huo, mwanahabari wetu aliyekuwa akifuatilia tukio zima kuanzia mwanzo hadi mwisho, alizungumza na Mbongo Fleva huyo ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Nawashukuru sana madaktari wa TMJ kwa kuweza kufanikisha upasuaji huu, Mungu awabariki sana. Ugonjwa ulianza kama miaka miwili hivi iliyopita lakini nilishindwa kufanya upasuaji kwani shoo zilikuwa zinabana, safari hii nikaona bora tu nifanye maana niliambiwa nikiacha tatizo linaweza kuwa kubwa zaidi,” alisema Diamond.

MSIKIE DAKTARI BINGWA WA UPASUAJI
Ijumaa Wikienda halikuishia hapo, lilimtafuta Dk. Edward Wayi, Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Hospitali ya CCBRT ambaye pia huzunguka katika nchi mbalimbali za Afrika kutibu watu ambapo aliufafanua ugonjwa huo kitaalamu.
“Ugonjwa wa Foot Corn unapokuanza, dalili za awali ni maumivu makali ya mguu ulioathirika.
“Ugonjwa usipotibiwa, husababisha malengelenge ambayo hupasuka na kusababisha kidonda. Kidonda hicho kisipotibiwa, husababisha kuharibika kwa ngozi ya ndani ya mguu inayotenganisha mifupa ya mguu na ngozi ya ndani. Hali hii kitaalamu huitwa Bursitis.
“Mgonjwa akishafikia hatua hii, huwa kwenye hatari ya kupata tatizo lingine kubwa zaidi liitwalo Septic Arthritis ambapo bakteria huingia ndani ya mwili kwa kupitia kidonda, kusambaa kwenye mfumo wa damu na kwenda kujikusanya kwenye viungio vya mifupa (joints).
“Mgonjwa akifikia hatua hii, viungio vya mifupa huvimba na kupata maumivu makali mithili ya mtu anayechomwa na sindano au msumari. Hata hivyo, kwa kuwa maumivu huwa yanakuja na kukata, wengi hupuuzia na matokeo yake, ugonjwa huingia kwenye hatua ya hatari zaidi iitwayo Osteomyelitis.
“Katika hatua hii, bakteria huwa tayari wamepanda na kuingia ndani ya mfupa kisha kuanza kuushambulia kwa kasi.
Mgonjwa akishafikia hatua hii, huwa hakuna tiba nyingine zaidi ya mguu kukatwa. Nawashauri Watanzania kutopuuzia ugonjwa huu kwani tayari watu wengi wameshakatwa miguu kwa sababu ya kuchelewa kupata matibabu,” alihitimisha daktari huyo.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate