Kigogo mmoja wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, kitengo cha kupakua makontena (TICS) jijini Dar, James Wambura, hivi karibuni alipata wakati mgumu kufuatia mwanamke aliyejulikana kwa jina la Margaret, aliyeishi naye kwa miaka mingi bila kufunga naye ndoa, kufariki dunia na ndugu kumgomea kuzika wakisema si mkewe mpaka alipe mahari, Uwazi limeipata nzima.
Marehemu Magreth enzi za uhai wake.
Margaret (pichani) alifariki dunia Februari 21, mwaka huu katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar na kuzikwa Februari 26, 2015
kwenye Makaburi ya Kitunda Machimbo, Ilala jijini Dar huku kifo chake
kikidaiwa kilitokana na kunywa sumu!MKASA KAMILI
Ilidaiwa kuwa, Wambura na marehemu waliishi kwa miaka mingi na kujaliwa kupata watoto wawili ambao ni wakubwa lakini hakuwa amefunga ndoa na mwanamke huyo, hivyo kumwondolea sifa ya maamuzi ya wapi akamzike marehemu huyo.
“Ilikuwa siku ya mazishi pale Kitunda nyumbani kwa Wambura, ndugu wa marehemu wakasema wapi akazikwe ndugu yao ni uamuzi wao, kwa vile mwanaume huyo hakuwa ametoa mahari kwa familia ya marehemu, hivyo hakuwa mkewe.”
SHARTI NI MOJA TU
Ikazidi kudaiwa kuwa, mwanaume huyo aliambiwa kuwa, endapo atalipa mahari ataruhusiwa kumzika mama watoto wake huyo kwani atakuwa ameshaozeshwa kihalali.“Kuna ndugu mmoja alisema hata kwenye vitabu vya dini, imeandikwa mwanaume akishalipa mahari anakuwa ameshaoa mke, haya mambo ya sherehe ni siku hizi tu, lakini zamani haikuwa hivyo, mahari ilihesabika ni ndoa kamili,” kilisema chanzo chetu.
Kikaongeza kuwa, ilibidi Wambura akubali kulipa mahari na faini ambapo alitajiwa shilingi milioni tano (5,000,000), lakini baada ya ‘kulia hali’ aliambiwa atoe shilingi milioni mbili (2,000,000), akafanya hivyo.
KUNYWA SUMU HADI KIFO CHAKE
Marehemu Margaret alidaiwa kunywa sumu, Februari 15, mwaka huu katika kile kinachodaiwa kuwa ni kuchoshwa na hali ambayo haikuwekwa wazi. Alikimbizwa Zahanati ya Mission iliyopo Kitunda, Dar es Salaam ambako alipatiwa matibabu.
Hali yake ilipozidi kuwa mbaya, alihamishiwa Hospitali ya Dar Group, Dar ambako pia haikutengemaa na kupelekwa Muhimbili ambako jioni ya Februari 21, mwaka huu, alifariki dunia.
No comments:
Post a Comment