Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akipeana mkono wa kuagana na
Mganga Mfawidhi wa zahanati ya Chanika Dk Betha Sanga ambaye pamoja na
watumishi wengine sita wa afya wa Manispaa hiyo wamepata udhamini wa
Serikali ya Korea Kusini kupitia Shirika lake la Maendeleo KOICA kwenda
kuongeza ujuzi nchini Korea Kusini kwa ajili ya kuboresha huduma katika
hospitali itakayojengwa Chanika. Wengine ni Dk Agatha Shinyala na Dk
Mary Machemba wa Amana Hospitali. Nyuma ya Meya ni Afisa kutoka KOICA
Seongbeom Ktm.
Dk Iyyovngchan Ktm kutoka Shirika la Maendele la Korea (KOICA) akisisitiza jambo kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa wakati kwa kuagana na watumishi sita wa afya wa Manispaa hiyo waliopata nafasi ya kwenda kuongeza ujuzi nchini Korea Kusini chini ya ufadhiliwa KOICA kwa ajili ya kuboresha huduma katika hospitali itakayojengwa Chanika.Kulia kwa Dr Iyyovngchan ni Afisa kutoka KOICA Seongbeom Ktm na wengine ni watumishi wataokwenda Korea.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiagana na Afisa kutoka shirika la Maendeleo la Korea Kusini (KOICA) Seongbeom Ktm muda mfupi baada ya hafla ya kuwaaga watumishi sita wa wa afya wa Manispaa ya Ilala waliopata nafasi ya kwenda kuongeza ujuzi nchini Korea Kusini chini ya ufadhili wa KOICA kwa ajili ya kuboresha huduma katika hospitali itakayojengwa Chanika. Kati kati ni Dk Iyyovngchan Ktm kutoka KOICA.
No comments:
Post a Comment