EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, March 13, 2015

SKIMU YA MPUNGA KIROKA YAPATA UGENI MKUBWA‏

DSC_0576
Msimamizi wa mradi wa FAO kijiji cha Kiroka mkoani Morogoro, Ajuaye Sigalla, akitoa muhtasari wa maendeleo ya mradi FAO unaotekelezwa na wanakikundi wa Umoja wa Wakulima Kiroka (UWAKI) mbele ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Filiberto Sebregondi walipofanya ziara ya kugagua miradi yao ya maendeleo mkoani Morogoro.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog)
Na Mwandishi wetu, Morogoro
BALOZI wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi ametembelea skimu ya umwagiliaji ya Kiroka na kusema kwamba atahakikisha kwamba kwa kushirikiana na wadau wengine ikiwamo serikali wataendelea kusaidia wananchi kujiinua kiuchumi.
Akiwa katika skimu hiyo inayosaidiwa na Shirika la Chakula duniani (FAO) ametaka miradi ya maendeleo nchini kutowaacha nyuma wanawake na watoto kwani wao ndio msingi wa maendeleo ya kijamii kuanzia ngazi ya kaya hadi Taifa.
Balozi huyo ambaye anatarajiwa kurejea Ulaya mwaka huu baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi nchini amesema kwamba kuwapo kwa asilimia 60 ya wafaidika na mradi huo wa Mpunga kuwa wanawake kumesaidia sana kuamsha maendeleo ambayo yanatakiwa kuendelea kusimamiwa.
"Wanawake wamefanikiwa kupeleka watoto wao shuleni. kuwapatia chakula kinachostahiki na kupata kipato na katika hili ni vyema wasiachwe nyuma kimaendeleo" alisema balozi huyo.

DSC_0633
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Filiberto Sebregondi akizungumza na wanakikundi wa Umoja wa Wakulima Kiroka (UWAKI) wanaofadhiliwa na FAO wakati wa ziara ya kutembelea miradi inayofadhiliwa na wadau wa maendeleo ambapo mradi wa Kiroka unafadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la FAO huku mradi wa makazi mapya kwa waathirika wa mafuriko Kilosa ukifadhiwa na Ubalozi wa Umoja wa Ulaya. Kushoto kwake ni Msimamizi wa mradi wa FAO kijiji cha Kiroka mkoani Morogoro, Ajuaye Sigalla.
Alisema kwamba amefurahishwa sana na mradi huo na kusema kwamba Umoja wake utaendelea kushirikiana na mashirika ya Umoja wa Mataifa na serikali katika kuhakikisha kwamba mwananchi wa kawaida wa Tanzania anapata maisha bora.
Mradi wa Kiroka ambao unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya FAO na benki ya NMB ikishirikiana na RaboBank umelenga kuboresha kilimo cha Mpunga na pia kuwawezesha wakulima hao kuwa na nafasi ya kupata fedha za kuendeleza majukumu yao.
Ili kufanikisha hilo wakulima wanapatiwa elimu ya fedha na pia utunzaji wa nafaka wa pamoja na mikakati ya mauzo.
DSC_0643
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Filiberto Sebregondi akifafanua jambo wakati akitoa salamu kwa wanakikundi wa Umoja wa Wakulima Kiroka (UWAKI). Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa kijiji cha Kiroka, Mbaraka Mnebe, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez pamoja na Msimamizi wa mradi wa FAO kijiji cha Kiroka mkoani Morogoro, Ajuaye Sigalla.
Mradi huo ulioanza 2004 na kutarajiwa kuisha Juni mwakani unatekelezwa 2018 umelenga kufungua fursa kwa wanawake na wanaume na kuongeza uzalishaji, kusaka masoko, kupata njia ya kupata mikopo na kujenga uwezo wa kufanikisha shughuli za maendeleo kwenye skimu.
Mradi huo unatarajiwa kutumia dola za Marekani 737,000 hadi utakapokamilika.
Wakizungumza na balozi huyo kuelezea mazingira yao wakulima walishukuru msaada unaotoka katika mashirika ya kimataifa na kuwaomba kusaidia kuwapatia fursa zaidi za maendeleo kwa elimu wanayoipata.
Wamesema mabadiliko yaliyosababishwa na elimu yamewafanya wazalishe Mpunga kwa wingi katika eneo dogo na kufungua fursa za masoko kwa hifadhi na utafutaji masoko wa pamoja.
DSC_0595
Katibu wa Umoja wa Wakulima Kiroka (UWAKI), Muhidin Kigadu akielezea mafanikio waliyoyapata tangu walipoanza kupewa mafunzo ya kilimo bora yanayofadhiliwa na Shirika la FAO mbele ya ugeni huo.
Mradi huo ambao ulianza na Watu wa Sua kama watoa elimu sasa wanapigwa msasa na Taasisi ya maendeleo mjini na Vijijini (RUDI) kwa lengo la kuhakikisha kwamba wanatumia mfumo wa Asia wa ulimaji wa Mpunga kwa kutumia maji kidogo huku wakihifadhi ghalani kusubiri bei nzuri.
Katika ziara hiyo ya karibuni ya Balozi huyo akiambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, viongozi hao walipata nafasi ya kusikiliza changamoto za wakulima katika mradi huo ambapo uzalishaji sasa umeongezeka kutoka gunia tano kwa eka kufikia gunia 25 kwa kulima kitaalamu.
Katibu wa Umoja wa Wakulima Kiroka (UWAKI), Muhidin Kigadu alisema mradi huo ambao ulianza Februari 21,2012 umewajengea uwezo wakulima wa mlimani kutengeneza makinga maji huku wakulima wa kwenye skimu wakilima kilimo cha mashadidi.
IMG_9373
Mwenyekiti wa kijiji cha Kiroka, Mbaraka Mnebe akielezea jinsi skimu ilivyowasaidia kuinua maisha ya wananchi kwa kuwapatia elimu iliyowaletea mafanikio makubwa yaliyowezesha kulima kisasa na kubadilisha maisha yao hasa katika makazi na huduma za jamii na kuwapeleka watoto shule.
Alisema wanawashukuru wahisani kwa kuwawezesha kurejesha uoto wa kijani ikiwa na pamoja na kuwa na kilimo cha matunda.
Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Kiroka, Mbaraka Mnebe amesema skimu imewasaidia kuinua maisha ya wananchi kwa kuwapatia elimu iliyowaletea mafanikio makubwa yaliyowezesha kulima kisasa na kubadilisha maisha yao hasa katika makazi na huduma za jamii na kuwapeleka watoto shule.
Aidha wakulima wamefanikiwa kununua vyombo vya usafiri vya moto kama Pikipiki na kuachana na Baiskeli.
DSC_0607
Mwanachama wa Umoja wa Wakulima Kiroka (UWAKI), mkoani Morogoro, Bi. Asha Bogasi akitoa ushuhuda jinsi maisha yao yalivyobadilika mpaka wanaweza kusaidia na waume zao kusomesha watoto wao kutokana na skimu ya mradi huo.
Hata hivyo amesema pamoja mafanikio hayo wanachangamoto hasa ya masoko na elimu ambayo wanadhani wanaihitaji zaidi huku akisisitiza zaidi kwamba elimu inatakiwa hata kama wamemaliza mradi na wahisani kuondoka.
Mradi bado ambao haujakamilika kwani kati ya hekta 147 za mradi ni kama hekta 40 zinazotumuka kwa kuwa miundombinu haijatawanyika vya kutosha katika hekta zote.
DSC_0661
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akijibu hoja mbalimbali zilizotolewa na kuwapa pongezi za kuweza kubadilisha maisha yao kupitia kilimo cha kisasa kinachofadhiliwa na FAO kwa wanachama wa Umoja wa Wakulima Kiroka (UWAKI) alipofanya ziara ya kukagua mradi huo kijijini hapo.
DSC_0588
Wanachama wa Umoja wa Wakulima Kiroka (UWAKI) wakiwa wamekusanyika kwenye shule ya msingi Kiroka wakati wa ugeni wa Shirika la Umoja wa mataifa na Ubalozi wa Umoja wa Ulaya ulipowatembelea kukagua miradi yao.
DSC_0573
DSC_0647
Mratibu mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na Balozi wa Umoja wa Ulaya wakiondoka kijijini hapo mara baada ya kukutana na kuzungumza na Wanachama wa Umoja wa Wakulima Kiroka (UWAKI).

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate