EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, March 26, 2015

UGUMBA WAMTESA WEMA

POLE sana! Tatizo la kutoshika mimba (infertility) au kushindwa kupata mimba (conceive) limekuwa likimtesa staa wa Bongo Movies, Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu na limehusishwa na ugumba.
Akizungumza na Amani juu ya ishu hiyo hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Wema alisema suala la kutopata mtoto limekuwa likimkosesha amani katika maisha yake ya ukubwani.
Staa wa Bongo Movies, Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu.
ASHINDA AKILIA
Alisema kwamba, amekuwa akishinda akilia kila anapokutana na shosti wake wa sasa, Aunt Ezekiel ambaye ni mjamzito.Wema alitiririka kwamba, kila wakati amekuwa akimwambia Aunt kuwa na yeye anatamani kupata mimba lakini Mungu hajamjalia. Kwa kusema hivyo, huwa wanajikuta wakikumbatiana na kuangua vilio wote kwa pamoja.
TATIZO UMRI UMEENDA
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa mkali huyo wa sinema za Kibongo ambaye pia ni Miss Tanzania 2006, mwanadada huyo anaona umri umeenda sana kwani tayari ana miaka 26 sasa.
“Unajua Wema alishajaribu kupata mtoto mara kadhaa ikashindikana na umri nao unakwenda hivyo lazima akose amani. Hebu fikiria aliwahi kuwa na Kanumba (marehemu Steven), Jumbe (Yusuf), Chaz Baba (Charles Mbwana) na Diamond (Nasibu Abdul) lakini kote huko alitoka kapa.
Lady jaydee.
YAMKUTA YA JIDE
“Mbaya zaidi ni maneno yanayosemwa na watu yanamuumiza sana, wanasema ni mgumba kama ilivyokuwa kwa Jide (mwanamuziki Judith Wambura ‘Jaydee’).“Kwa kweli hali hiyo inamtesa sana ila watu hawajui bora wakafunga vinywa vyao na kuacha kuandika kwenye mitandao ya kijamii,” alifunguka mtu huyo wa karibu.

AKIWAONA MA-MISS TZ WENZAKE WANA WATOTO KILIO
Chanzo hicho kiliendelea kufunguka kwamba, Wema amekuwa akilia kila anapowaona ma-Miss Tanzania wenzake wakiwa na watoto wao.
Ilisemekana kwamba warembo ambao wanamliza ni Wema Nancy Sumary (Miss Tanzania 2005), Faraja Kota (2004), Hoyce Temu (1999), Jacqueline Ntuyabaliwe ‘K-lynn’ (2000) na Miriam Gerald (2009).
Ilisemekana kwamba wengine aliokuwa nao kwenye shindano hilo mwaka 2006 ambao wana watoto ni Lisa Jensen, Aunt Ezekiel na wengine ambao kwa pamoja wamekuwa wakimfanya naye atamani kupata mtoto.
DAKTARI AELEZA
TATIZO KWA KINA
Akielezea tatizo hilo kwa kina, Dk. Fadhili Emily wa Kitengo cha Tiba ya Sayansi cha The Fadhaget Sanitarium Clinic kilichopo Mbezi-Africana jijini Dar alisema:“Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, wanandoa asilimia 50 wanapata mimba ikiwa watajamiiana bila kutumia kinga, wakifanya tendo hilo ndani ya miezi mitatu, asilimia 75 baada ya miezi sita na asilimia 95 baada ya mwaka mmoja lazima kuwe na matokeo kama hakuna kuna tatizo.
Aunt Ezekiel.
NINI SABABU?
“Sababu za tatizo la kutopata mimba ni nyingi sana na baadhi yake ni hizi zifuatazo:
“Matatizo ya mbegu za kiume (sperm disorders).
“Asilimia 35 ya wanaume wana tatizo hili na lingine ni kutopevuka kwa mayai kwa wanawake kitaalam huitwa ovalatory dysfunction.
“Matatizo mengine ni yale yasiyo ya kawaida ya ute wa shingo ya uzazi ambapo ni asilimia 5 tu.
“Wengine huwa na matatizo ya homoni na wapo wanawake ambao hawapati mimba na sababu zao hazijulikani, hawa ni asilimia 10.”
MSONGO NA
WASIWASI
“Wengine ni kutokana na kuwa na msongo na wasiwasi. Tatizo lingine la mwanamke kutoshika mimba husababishwa na hitilafu katika mirija ya uzazi (tubal dysfunction), hawa huwa asilimia 30. Wanawake wenye tatizo hili wanashauriwa kuhudhuria kliniki za akina mama ili waonane na madaktari.
Lisa Jensen.
“Lakini pia wanashauriwa kufuatilia siku zao za mzunguko wa hedhi na tendo la ndoa mara kwa mara hasa baada ya siku 10 kutoka siku anapomaliza hedhi na aanzie siku ya kwanza ya kupata hedhi.
“Pia wanawake wanashauriwa wawe wanapima joto la mwili asubuhi na jioni kipindi cha kushika mimba na kama litaongezeka kwa nyuzi joto 0.5 wanashauriwa kipindi hicho kufanya tendo la ndoa.”
KWA ULAYA NA MAREKANI
“Kwa nchi za Ulaya na Marekani wana kipimo cha kuonesha siku ambayo yai litapevuka, hivyo mtu kuwa na uhakika na siku ya kupata mimba akiamua. Kipimo hicho kinaitwa luteinizing hormone prediction test kits.
“Pia wanawake wanaotaka kupata mimba wanashauriwa kuepuka ulevi na uvutaji wa sigara kupindukia. Lakini hata wale wenye mimba wanashauriwa kuepuka vitu hivyo.”
UGUMBA NA UTASA
Dokta huyo aliendelea mbele na kusema ugumba ni tatizo linaloweza kuondoka kwa mtu siku moja. Na mgumba ni mwanamke au mwanaume na ni yule mtu ambaye umri wake wa kuzaa umefikia lakini hawezi kutunga mimba (kwa mwanaume) au kutungwa mimba (kwa mwanamke).Alisema tasa ni viumbe wote, hata wanyama wanaweza kuwa tasa lakini wanyama hawawezi kuwa wagumba.
CHANZO:GPL

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate