Mwanahabari wetu aliyekuwa akikusanya matukio ukumbini humo, aliwashuhudia watu waliomzunguka Ray wakionesha hofu yao pale fulana yake ilipopanda juu na kuiacha bastola yake aliyoichomeka kwenye suruali ikionekana bila kificho ambapo zaidi walihofia mazingira ya unywaji wa pombe uliokuwepo.
“Jamani hii si hatari na ‘masanga’ haya anayogonga hapa ukimkorofisha hata kidogo tu si anaweza kukushuti bila kuwaza nini kitatokea?,” alisikika mmoja wa watu waliokuwa wamekaa jirani na msanii huyo.Baadhi ya watu hao waliokuwa jirani na Ray aliyekuwa amekaa pamoja na msanii mweziye Jacob Steven ‘JB’, walionekana wakiondoka eneo hilo kwa hofu ya usalama wao.
Mfano wa bastola ya Rey.
“Hapa si salama sana ndugu zangu bora tuondoke, unaweza hata
ukamkanyaga bahati mbaya akakulipua makusudi,” alisikika jamaa mwingine
aliyekuwa eneo hilo.Jitihada za mwanahabari wetu kuzungumza na Ray eneo
hilo hazikuweza kuzaa matunda kufuatia mazingira ya unywaji pombe
uliokuwepo, lakini alipotafutwa siku iliyofuata, simu yake iliita bila
kupokelewa.
No comments:
Post a Comment