Kwenu mastaa wa tasnia mbalimbali Bongo, habari zenu bwana. Poleni na majukumu ya kila siku ya kulijenga taifa.Mkitaka kujua afya yangu, mimi ni mzima, namshukuru Mungu naendelea kutimiza majukumu yangu, likiwemo hili la kuwaandikia barua.
Nimewakumbuka leo kupitia barua, nataka kuwaambia kwamba mimi pamoja na mashabiki wengine wa sanaa yenu tumewachoka. Tumechoka kuona na kusikia kila siku mkifanya maigizo kwenye maisha yenu halisi.
Hivi ni kwa nini kila kukicha tunasikia mnaachana? Kwa nini hamdumu kwenye uhusiano wa mapenzi? Kwa nini hamdumu kwenye ndoa kama mashabiki wenu wanavyowategemea?
Penzi linapoanza kushamiri, mnalinadi kwenye mitandao na vyombo vya habari. Mnawaaminisha mashabiki wenu kuwa mnapendana kwa kauli zenu motomoto lakini ndani ya miezi miwili mitatu penzi chali.Wengine mnaonesha kwamba mmedhamiria na kuamua kufunga ndoa kabisa, lakini kumbe moyoni bado mnakuwa mna lenu jambo. Mashabiki wenu wanafurahia kuona mmeoana lakini ndoa nayo haidumu, mnaachana.
Watu hawapendi kuona Nay wa Mitego na Siwema mkiwa mmeachana. Tena mnaachana kwa kupeana maneno yanayoonesha kwamba mlikuwa hamna nia ya dhati ya kuwa wapenzi.Shamsa Ford na Dick, kapo yenu ilikuwa nzuri. Mlipamba vyombo vya habari, uhusiano wenu ukazaa matunda ya mtoto mmoja lakini ndoto ya kuishi kama mume na mke imeyeyuka.
Nasibu Abdul !٪Diamond!& na Wema Sepetu penzi lenu lilikuwa likipendwa na wengi, likaishia njiani. Rose Ndauka na Malick Bandawe mlioishi na kubahatika kupata mtoto mmoja, nini kiliwakuta? Inasikitisha.Wolper na Dallas nao walipamba sana vyombo vya habari lakini mwisho wa siku chali. Ndugu zangu, mnapaswa kubadilika. Msiigize maisha yenu. Igizeni kwenye filamu, mkirudi nyumbani mjitambue kwamba heshima, upendo, busara vinahitajika ili kuishi na mwenzako.
Mbona
wapo wasanii wengi tu maarufu duniani na wamedumu kwenye uhusiano?
Kwa nini msiige mfano kwa mastaa kama Marlaw na mkewe, Jay Z na
Beyonce ambao wanaheshimu penzi lao hadi sasa?Jamani, cha msingi
mnapaswa kuheshimu suala la uhusiano, msifanye masihara katika maisha
ya ukweli. Vitu vingine vinapaswa kufanyika kwenye filamu pekee na
siyo kuvihamishia katika maisha halisi.Bila shaka mtakuwa mmenielewa na mtabadilika, kila la kheri.
No comments:
Post a Comment