Friday, May 29, 2015
SABABU 10 ZA MASTAA WA KIKE KUTODUMU KWENYE NDOA!
Na Hamida Hassan
Mastaa wengi wamekuwa hawadumu kwenye ndoa zao na wengine kwenye uhusiano wao wa kimapenzi. Ukijaribu kumuuliza kijana yeyote mwenye nia ya kuoa atakuambia bora aoe mwanamke wa kawaida kuliko staa.
Si suala la kuoa tu, hata kwenye mapenzi ya kawaida ni wachache wanaoanzisha uhusiano na mastaa wakiwa na ndoto za kudumu kwa muda mrefu. Ukiona kijana ‘anamsalandia’ staa ujue ni ili amuonje tu kisha amtose.
Pia ukifuatilia utagundua kuwa, mwanamke wa kawaida akitokea kumpenda staa wa kiume, anatafuta ile sifa ya kuwa naye lakini anajua hawezi kudumu naye.Kutokana na hilo sasa, makala haya yanajaribu kukupa kwa ufupi sababu 10 ambazo zinawafanya mastaa wengi wa kike kutodumu kwenye ndoa.
Tamaa
Hili lipo sana kwa mastaa wa kike. Baadhi yao wana tamaa ya kuwa na maisha f’lani ili waonekane nao wamo wakati uwezo haupo. Matokeo yake sasa akiolewa na mwanaume ambaye hana kitu, akimpata wa pembeni ‘pedeshee’ wa kumtunza, kwa tamaa zao hujikuta wakisaliti.
Unakuta msichana kwa kuwa ni staa, anataka awe na gari zuri, abadili nguo kila siku, simu kali na vitu vingine vya thamani wakati pesa hana na mume naye ni kapuku. Hapo ndipo wengi huamua kuchepuka na matokeo yake sasa hajali tena ndoa.
Ustaa mwingi
Mastaa wengi wakishajitambua kuwa wao maarufu, basi hata kwa wapenzi wao wanaleta zile nyodo za ustaa. Wanasahau kuwa hata rais anapokuwa na mkewe humnyenyekea kama mke na mambo mengine kuendelea.
Utakuta staa anataka kuonesha ustaa wake kwa mumewe, yaani anataka mume awe chini yeye awe juu kisa tu anatikisa jiji.
Unyenyekevu katika mapenzi unakuwa haupo, eti anajipa imani kwamba hata akiachwa kwa kuwa anapapatikiwa na wanaume wengine kutokana na ustaa wake, hatakosa wa kumchukua. Hiyo ni dhana potofu!
Uvivu, kupenda kulala…
Baadhi ya mastaa hata wakiolewa wanashindwa kuvaa joho la ‘mke wa mtu’. Wanapenda kukaa tu na kuletewa kila kitu nyumbani. Akicheza muvi moja na kujulikana basi anaona dunia ndiyo yake, hakumbuki kutafuta kazi ya uhakika.
Usiku atapenda atoke, mchana ni mtu wa kulala tu kisa kachoka. Ni mwanaume wa aina gani atakayemvumilia?
Starehe kwa sana
Mke wa mtu hata kama anastahili kustarehe siku mojamoja, lakini baadhi ya mastaa walioingia kwenye ndoa huona wao starehe lazima ichukue sehemu kubwa ya maisha yao. Atalazimisha kila siku watoke na hata kama mume atakuwa si mtu wa kuendekeza mambo hayo, yeye ataomba awe anaenda na mastaa wenzake, akikataliwa inakuwa tatizo.
Hawajitambui
Mastaa wengi wanakosa elimu ya kujitambua. Ndiyo maana wengi wanaitwa malimbukeni. Unakuta staa amepata mume mzuri tu lakini yeye anashindwa kujitambua kuwa yeye ni mke wa mtu asiyestahili kuingiza ustaa wake kwenye maisha yake ya nyumbani.
Ndoa fasheni
Jaribu kuchunguza utagundua kuwa, mastaa wengi wanaolewa kama fasheni. Utamkuta staa wa kike anasema wazi kwamba, amechangia wengi sana hivyo na yeye anataka kuchangiwa hivyo analazimisha kuolewa.
Wanaoolewa kwa sababu hiyo ni wale ambao hata ndoa zao zikivunjika hawaoni hatari, wanaona ni sawa tu kwa sababu angalau wameonja ndoa!
Uvumilivu wa shida
Mara nyingi watu wanapooana hukubaliana kuishi pamoja kwa shida na raha. Mastaa wengi hawataki shida, wao wanataka raha tu.
Matokeo yake sasa ukiona mambo yanaenda kombo, ni wachache sana wanaoweza kuvumilia shida. Wengi wataanza visa na hatimaye wataomba talaka au kuamua kutoka kwenye ndoa!
Dhana potofu
dhidi yao
Mastaa wengi wanaonekana si watu wa kuolewa. Sasa anapotokea mwanaume wa kumuoa staa, hata kwenye mambo ya kawaida ataona anafanyiwa hivyo kwa sababu ya ustaa.Matokeo yake sasa, hata kama staa huyo atajitahidi ili adumu kwenye ndoa yake atashangaa ile damu ya ustaa inamtesa.
Wanakosa staha
Mke kama mke lazima awe na staha, kitu ambacho baadhi ya mastaa wanakikosa. Utakuta staa kaolewa lakini ana marafiki wengi wa kiume na anataka mume wake asihoji juu ya urafiki wao.Kama ni msanii akiwa lokesheni, afanyiwe lolote na wanaume, avae nguo hata za utupu kisa eti anaigiza. Mbaya zaidi si lokesheni, hata nje ya fani wanataka kuishi kisanii.
Wako tayari kuachika
Mastaa wengi wa kike wakiolewa, wanakaa mkao wa kuachika wakati wowote. Ni wachache wanaofanya jitihada za kutunza ndoa zao. Yaani wanatembea kwenye ile dhana potofu kwamba staa hawezi kudumu kwenye ndoa.
Sababu hizo hapo juu na nyinginezo ndizo zilizosababisha ndoa za mastaa kama vile Nuru Nasoro ‘Nora’, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’, Jack Patrick, Aunt Ezekiel’, Salome Urasa ‘Thea’, Halima Yahaya ‘Davina’, Judith Wambura ‘Jide’, Stara Thomas na wengineo kuvunjika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
HABARI MBALIMBALI
‘Dk. Cheni’
‘Sharo Milionea
‘Thea’
African Women
AGNESS MASOGANGE
AK CLASSIC COSMETICS
ALI KIBA
Amanda Poshy
Ant
ANT LULU
Ashley Toto
Aunt Ezekiel
Aunty Ezekiel
AUNTY LULU
Azam Fc
Baby Madaha
BAHATI BUKUKU
Barnaba
BATULI
BBA
Beauty of the day
Belle 9
BI KIDUDE
BIBI BOMBA
Big Brother
Big Brother Africa
Bill Gates
BINTI KIZIWI
BOB JUNIOR
Bodi ya Filamu
Bongo Movie
Bongo Movies
CCM
CHADEMA
Chombezo
Christina Shusho
Chuchu hans.
Clouds Media Group
Club Bilicanas
DAR LIVE
DAVINA
Dayna Nyange
Diamond
Dida
Diva Loveness Love
Dj Ommy Crazy wa Maisha Club
DOGO JANJA
DOKI
DR.CHENI
DSTV
Dude
Dully Sykes
EBSS 2013
Elizabeth Michael
Epiq Bongo Star Search (EBSS)
ESHA BUHETI
Ester Bulaya
Feza Kessy
FIESTA 2014
Flaviana Matata
FLORA MBASHA
FLORA MVUNGI
Francis Cheka
GARDNER
GLOAL PUBLISHERS
GLOBAL TV ONLINE
H. BABA
Halima Mdee
HAMISA
Happy birthday
Hemedi
Hemedy Suleiman
HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE
Hoyce Temu
Huddah Monroe
HUSINA
IRENE PAUL
Irene Uyoya
ISABELLA
J film 4 life
Jack Chuz
JACK PATRICK
Jacob Steven ‘JB’
Jacqueline Dustan
JACQUELINE WOLPER
Jaji Khamis 'Kashi'
Jay Dee
JENNIFER KYAKA (ODAMA)
JIDE
JINI KABULA
JK
JO
Johari
Jokate Mwigelo ‘Kidot’.
JOTI
Joyce Kiria
Joyce Kiwia
JUX
K-LYNN
KADINDA
kaja
Kajala Masanja
Kapotive Star Singers
KATUNI
Kemmy
Kero Zetu
KHADIJA OMAR KOPA
KIKWETUKWETU
KILI MUSIC AWARDS
KOLETA
Lady Jay Dee
Lady Jaydee
Lake Oil
LAVEDA
Linah Sanga
Linex
Lisa Jensen
Loveness Diva
Lucy Francis Komba
Lulu
M2 The P
MABILIONEA
Madam Rita
MADELA
Magazeti
Mahusiano
Maimartha Jesse
MAINDA
MAISHA
Makala
Malkia Elizabeth
MAMTEI
MANDELA
MARIAM ISMAIL
Masanja Mkandamizaji
Mashindano ya Miss Tanzania
Matangazo
Matonya
MaxMalipo
MAYA
MELLIS EDWARD
MENINAH
MGOSI MKOLONI
Mh Halima Mdee
mic
Michezo
MILLEN HAPPINESS MAGESE
MISS CHANG'OMBE
MISS DAR CITY CENTER
Miss East Africa
MISS REDD'S IRINGA 2013
MISS TANGA 2013.
MISS TANZANIA 2014
Miss Tanzania mwaka 2011
MISS TEMEKE 2014
MISS USTAWI
MISS UTALII TANZANIA 2012/13
Miss vyuo vikuu 2013
MKALA
MREMBO HUDDAH
Mrisho Mpoto
Mrisho Ngassa
MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES.
MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013
Mtitu
muziki
Mwana FA
MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14
Mzee Majuto
Nancy Sumari
Nani Mtani Jembe?
NAPE
Nassoro ‘Nora’
Natasha
Nay wa Mitego
Necta
Nelly Kamwelu
NEY WA MITEGO
Nisha
NSSF;Zantel
Nyamwela
NYimbo
Nyota yako
OBAMA TANZANIA
OMMY DIMPOZ
P FUNK
PAM D
Peniel Mgilwa ‘Penny’
PETIT MAN
Profesa Jay
Q - CHILA
Q Boy
Q Chilla
QUEEN DARLEEN
RACHEL NDAUKA
RAIS KIKWETE
Rais Kikwete.
Rasimu Ya Katiba TZ
Ray
Ray C
Redd’s Miss IFM
REDD'S MISS KAGERA 2013
REDD'S MISS TZ
REDDS MISS TANZANIA 2014
Redds Miss wa Mikoa
REHEMA FABIAN
RICHIE RICHIE
Rihanna
ROSE MUHANDO
Rose Ndauka
Ruge Mutahaba.
SABASABA 2013
Saida Karoli
Saikolojia
Sajeti
SAJUKI
Sandra
SHAA
Shamsa Ford
Sheikh Ponda
Shilole
Sintah
Siwema
Skin Tricks
Snura Mushi
Spika Makinda
staa
Staa Wetu
Stella Mwangi
STYLE ZA NYWELE
Taifa Stars
Tamasha la matumaini
TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013
Tangazo
TANZANIA
TEGO
TENGENEZA WEBSITE NA BLOG
TID
Tundaman
Tupo wangapi?
TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14
Twanga Pepeta
USA PAGEANT 2014
VAI
Wastara
WEMA
WEMA SEPETU
Yanga
Yanga Bingwa 2013
YOUNG D
Yvonne Cherry ‘Monalisa’
Z Anton.
Zari
Zito kabwe
No comments:
Post a Comment