EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, May 11, 2015

SIWEMA WA NAY MBARONI!

Baltazar Mashaka, MWANZA
Mzazi mwenzake staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Siwema Edson (27) ametiwa mbaroni na kusota rumande kwa siku kadhaa akidaiwa kujipatia mali kwa njia ya vitisho kutoka kwa kigogo mmoja serikalini (jina linahifadhiwa kwa sasa).
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi, Charles Mkumbo.
Mei 2, mwaka huu, Siwema alilala ‘nyuma ya nondo’ (mahabusu) kwa siku mbili katika Kituo Kikuu cha Polisi, Wilaya ya Nyamagana jijini hapa baada ya kukamatwa nyumbani kwake Lumala, Manispaa ya Ilemela.
Aliyekuwa mchumba wa Ney wa mitego Siwema Edson akiwa katika Pozi.
KISA KAMILI
Kwa mujibu wa chanzo, awali ilidaiwa kuwa, Siwema aliingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na kigogo huyo jijini hapa kwa ahadi ya kufunga naye pingu za maisha kufuatia kigogo huyo kufiwa na mkewe.

Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego.
YALIYOJIRI NDANI YA UHUHUSIANO SASA
Ikazidi kusemekana kwamba, wawili hao wakiwa ndani ya uhusiano, Siwema hakuwahi kumfahamisha kuwa ana mchumba ambaye ni Nay. Ikafika mahali, kigogo akamvisha pete ya uchumba, picha zikatoka kwenye gazeti moja (siyo la Global Publishers).
NAY AGUNDUA, AJA JUU
Ilizidi kuelezwa kuwa Nay baada ya kugundua kuwa Siwema amevishwa pete ya uchumba na kigogo huyo, alihamanika kiasi kwamba taarifa zilimfikia kigogo huyo wa serikali naye akaamua kujitoa kwa Siwema, akaoa mwanamke mwingine.
“Tatizo Siwema hakuwa muwazi  kwa kigogo kwamba, Nay ni mchumba wake. Lakini kabla ya kigogo kumtema Siwema, kumbe alishawahi kumpiga picha za utupu mwenyewe akiwa hajui.”
 BAADA YA SIWEMA KUMWAGWA
“Sasa baada ya Siwema kumwagwa kutokana na kelele za Nay kwamba demu ni mchumba wake, ndipo zile picha Siwema alizitumia kumtishia amnunulie gari vinginevyo angemwanika kwa kuzitupia kwenye mitandao ya kijamii ya Instagram na Facebook,” kilieleza chanzo hicho.
KIGOGO ATISHIKA, AINGIA MKENGE
Ikazidi kuelezwa kuwa, aliposikia vitisho hivyo, kigogo huyo aliamua kumweleza mkewe juu ya sakata zima ambapo walikubaliana kumnunulia Siwema gari na akampa na kiasi cha fedha kwa masharti ya kuzifuta picha hizo kutoka kwenye simu yake.
“Lakini Siwema licha ya kununuliwa gari aina ya Honda CRV na akapewa na kiasi cha fedha alichotaka, bado hakuzifuta picha hizo kwenye simu yake.
“Kana kwamba haitoshi, aliendelea kumtishia tena ambapo safari hii alitaka  atumiwe kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya mtaji wa biashara, jambo lilimnyong’onyeza kigogo huyo na kuamua kwenda kutoa taarifa kwenye vyombo vya dola kwa hatua za kisheria,” kilisema chanzo.
KAMANDA WA POLISI SASA
Akizungumza na Ijumaa Wikienda mwishoni mwa wiki iliyopita, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi, Charles Mkumbo alikiri kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo.
Alisema Siwema alikamatwa baada ya mlalamikaji kutoa taarifa kwa jeshi hilo ambapo walifungua jalada la uchunguzi Mei 2, mwaka huu na siku hiyohiyo walimkamata mtuhumiwa akiwa nyumbani kwake, Lumala Manispaa ya Ilemela.
“Ni kweli tulimkamata Siwema Edson (27), mkazi wa Lumala. Ametuhumiwa kujipatia mali kwa njia ya vitisho. Awali alikuja mlalamikaji kabla ya kukamatwa.
“Hawa watu awali walikuwa wapenzi. Katika mapenzi yao, siku moja, Siwema alimpiga picha za utupu mlalamikaji bila yeye kujitambua wala ridhaa yake,” alisema DCP Mkumbo.
Alisema baadaye uhusiano wao ulivunjika, ndipo Siwema akatumia picha hizo kumtishia kuwa kama hatatimiza matakwa yake kwa kumnunulia gari na kumpa fedha, basi angezisambaza picha hizo kwenye mitandao ya kijamii ya Instagram na Facebook.
“Mlalamikaji alitimiza matakwa ya mtuhumiwa kwa kumnunulia gari aina ya Honda CVR lenye namba za usajili T103 DDU na akamtumia na fedha. Lakini Siwema aliendelea kumtumia vitisho, akimtaka amtumie kiasi kikubwa cha fedha za mtaji, ndipo mlalamikaji akaja kutoa taarifa polisi, likafunguliwa jalada la uchunguzi na siku hiyohiyo akakamatwa,” alisema DCP Mkumbo.
Aliendelea kusema kuwa, kwa sasa gari hilo linashikiliwa kituoni hapo huku Siwema akiachiwa kwa dhamana wakati upelelezi ukiendelea. Ukikamilika atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.
 SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO
Hivi karibuni, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete alisaini sheria ya makosa ya mtandao.
Sheria hiyo, inakataza mtu kutumia mitandao kwa nia ya  kumchafua mtu au kuanika picha zake, hasa za utupu  bila ridhaa yake.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate