Jana
jumapili tarehe 24, Mei 2015 Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira
wa Miguu nchini TFF imeketi katika ukumbi uliopo makao makuu ya
Shirikisho uwanja wa Karume.
Kamati ya Utendaji imepitia masuala mbalimbali na kutoa maamuzi yafuatayo:
CLUB LICENCING (Leseni za vilabu)
Kamati ya Utendaji imeiagiza sekretarieti ivisisitize vilabu vya Ligi Kuu umuhimu wa kukamilisha maombi yao ya ushiriki wa ligi kuu kwa msimu wa 2015/16 kwa kuwasilisha fomu za maombi ya Leseni za vilabu TFF. Klabu ambayo haitakamilisha mchakato huo haitaruhusiwa kushiriki ligi kuu ifikapo msimu wa 2015/16.
KOMPYUTA - Kutokana na maamuzi ya mkutano mkuu wa TFF uliofanyika Morogoro ambao uliagiza wanachama wake wapya wapewe kompyuta, agizo hilo limetekelezwa na kompyuta hizo watakabidhiwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji wanaotoka kanda hizo ili waziwakilishe maeneo husika. Mikoa hiyo ni Geita, Katavi, Manyara, Njombe na Simiyu.
MFUKO WA FDF - Kufuatia mkutano mkuu wa TFF kuingiza kipengele cha FDF katika katiba yake, kikao cha Kamati ya Utendaji wa mujibu wa katiba kimepitisha kanuni za uendeshaji wa mfuko huo.
Aidha kikao hicho kimeteua wajumbe wafuatao wawe wajumbe wa tume hiyo
(i)Tido Mhando - Mwenyekiti,
(ii) Deogratius Lyatto - Makamu mwenyekiti
(iii)Ephraim Mafuru - mjumbe,
(iv)Beatrice Singano - mjumbe,
(v)Joseph Kahama - mjumbe
(vi)Ayoub Chamshana - mjumbe.
Pia Henry Tandau ameteuliwa kuwa katibu mtendaji wa mfuko huo.
AJIRA
Kamati ya Utendaji ya TFF imemteua Boniface Wambura kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Bodi ya Ligi Kuu nchini kuanzia tarehe 01, Juni 2015. Wambura kabla ya uteuzi huo alikua mkurugenzi wa mashandano TFF.TFF inampongeza Wambura kwa uteuzi na inaamini atatoa mchango mzuri katika kukuza na kuzitangaza ligi zetu.
Kamati ya utendaji imemteau Martin Chacha (mratibu wa timu za Taifa) kukaimu nafasi ya mkurugenzi wa mashandano TFF.
TIMU ZA TAIFA
Kamati ya utendaji ya TFF imesikitishwa na mwenendo mbovu wa Taifa Stars Rais wa TFF, Jamal Malinzi kwa niaba ya kamati ya utendaji amewaomba radhi wapenzi wa mpira kwa matokeo mabaya ya Taifa Stars kwenye michuano ya Cosafa.
Kikao cha kamati ya utendaji kilipokea taarifa juu ya mwenendo wa timu ya Taifa.Baada ya majadiliano ya kina, ilikubaliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa, Mart Nooij apewe changamoto maalumu ya kufuzu kwa fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN na asipofanikisha jambo hilo mkataba wake utasitishwa mara moja.
Maamuzi haya yamezingatia hali halisi ya timu ya Taifa ambayo inakabiliwa na michuano mbalimbali ya kimataifa ndani ya kipindi kifupi. Aidha katika kuliimarisha benchi la ufundi la timu ya Taifa, Leopald Tasso Mkebezi ameteuliwa kuwa meneja mpya wa timu ya Taifa.
Mkebezi amewahi kuwa meneja wa timu ya Taifa katika kipindi cha mwaka 2006 - 2012.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO
LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

No comments:
Post a Comment