Mabingwa
wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2014- 2015, Yanga wakishangilia
ubingwa wao huo mara baada ya kumalizika kwa mtanange wao dhidi ya Azam
FC, uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam .Mtanange
huo ulimalizika kwa Azam kushinda Bao 2-1.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI,
MMG.
Mgeni
Rasmi katika Mchezo huo, Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,
Mh. Dkt. Fenella Mukangara akimkabidhi Nahodha wa Timu ya Yanga, Nadir
Haroub cheti cha pongezi kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Soka Duniani,
Sepp Blatter kwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara 2014 -
2015.Kushoto ni Rais wa TFF, Jamal Malinzi na wa pili kulia ni
Mwenyekiti wa Yanga, Yussuf Manji.
Mgeni
Rasmi katika Mchezo huo, Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,
Mh. Dkt. Fenella Mukangara akimpongeza Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho
Ngassa baada ya kuchaguliwa kuwa Mchezaji bora wa mwezi wa nne.
Wachezaji
wa Timu ya Yanga wakiingia uwanjani tayari kwa kukipiga na timu ya Azam
FC katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, katika Uwanja wa
Taifa jijini Dar es salaam leo.
Mwali kabla ya kukabidhiwa kwa wenyewe.
Watu
wa huduma ya kwanza wakifatilia mchezo huku wakiangalia yule atakaeumia
na kwenda kumsaidia, hii ni kutokana na Mvua kubwa inayoendelea kunyesha
hapa jijini Dar leo.
Msambuliaji
wa Yanga, Mrisho Ngassa (kulia) akimkimbiza Kiungo wa Kati wa Azam,
Mudathir Yahya wakati wa mtanange wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara,
uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar. Azam
imeshinda bao 2-1.
No comments:
Post a Comment