Staa wa muziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond Plutnumz’.
Meneja wa msanii huyo, Babu Tale, awali aliulizwa na gazeti hili juu
ya kinachoendelea kuhusiana na vijana hao waliotimuliwa shule Aprili
mwaka huu kwa kutolipiwa ada, lakini akionekana kupatwa na jazba,
alisema wanasikitishwa na jinsi wazazi wa watoto hao wanavyokiuka
makubaliano, hivyo wao hawataki tena kusema lolote kwa sasa.“Kama wao wanadhani kwa kwenda kwenye media (vyombo vya habari) ndiyo watoto wao watasomeshwa, basi na waende hukohuko watasomeshewa watoto wao,” alisema Tale aliyeonekana kukasirishwa na mwendelezo wa habari hiyo.
Tale alitoa kauli hiyo kufuatia mmoja wa wazazi hao wa watoto Hillary na Hamis, kudai kuwa hakuna maendeleo yoyote ya kulipiwa ada kwa vijana wao, kwani ingawa waliambiwa mambo yangekuwa sawa baada ya siku chache, lakini danadana zinaendelea.
Mwanasheria mmoja maarufu nchini aliyeomba hifadhi ya jina lake, aliliambia gazeti hili kuwa endapo wazazi wa vijana hao wataamua, sheria zinawaruhusu kumpeleka mahakamani msanii huyo kwa kukiuka mkataba, hata kama haukuandikwa.
“Makubaliano ya mdomo ni mkataba unaotambuliwa kisheria, mradi tu wazazi waweze kuthibitisha, tena kwa hili, inaonyesha siyo tu mkataba, bali inaonyesha Diamond hakufanya hivyo kwa mapenzi yake kwa watoto, bali baada ya wao kumfanyia kitu, aliwapeleka shule kuonyesha u-siriazi aliokuwa nao juu ya ahadi hiyo,” alisema mwanasheria huyo.
Januari mwaka jana, Diamond aliendesha shindano kwa watoto la kucheza mtindo wa Ngololo na kuahidi zawadi kwa washindi katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar. Vijana hao walioshinda, walipewa ofa ya kusomeshwa katika shule hiyo hadi kumaliza elimu yao ya msingi, lakini tangu wapelekwe hawajawahi kulipiwa ada.
No comments:
Post a Comment