Baadhi ya washiriki wa shindano
hilo wakiwa kwenye pozi la pamoja ndani ya Hoteli ya Colloseum maeneo ya
Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa mashindano hayo Jacqueline Chuwa (katikati) akizungumza jambo mbele
ya wanahabari waliokuwa Hoteli ya Colloseum Mnazi Mmoja jijini Dar.
Kushoto ni Mkuu wa Itifaki wa mashindano hayo Angerls Faber na Mratibu
wa Shindano hilo Sebu Panya.
Angerls Faber akielezea namna mashindano hayo yatakavyo kuwa.
Baadhi ya waandishi wa habari, mamiss na waandaji wa shindano hilo.
SHINDANO la kumsaka mlimbwende atakayeuwakilisha
Mkoa wa Kilimanjaro kwenye shughuli mbalimbali za Kijamii limezinduliwa
mapema leo, ambalo litakuwa na jumla ya washiriki 20 watakaowania taji
hilo Julai 24 mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Kili Home Resort.Akizungumza katika uzinduzi huo mbele ya waandishi wa habari katika Hoteli ya Collosseum Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, mkurugenzi wa mashindano hayo ambaye ni Miss Kilimanjaro 2008 Jacqueline Chuwa amesema kwamba mashindano haya ni ya kipekee kabisa kwani hayahusiani na mashindano ya umiss ya aina yoyote kwani yamesajiliwa maalumu kwa mkoa wa Kilimanjaro.
“Nimeamua kuanzisha mashindano haya ili mkoa wangu wa Kilimanjaro uweze kuwa unapata balozi wa kuiwakilisha jamii katika mambo mbalimbali yakiwemo ya Utalii ambao ndiyo dira kubwa ya mkoa wetu.
“Naomba Watanzania watambue kwamba shindano hili halihusiani na Shindano la Miss Tanzania kwani limesajiliwa maalumu kwa wakazi wa Kilimanjaro na ndiyo maana tumechagua warembo kutoka huko na si sehemu nyingine kama yalivyo mashindano mengine ya umiss,” alisema Chuwa.
(Habari/Picha: Musa Mateja)
No comments:
Post a Comment