Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MGOMBEA mpya wa urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli, kama akichaguliwa kuwa rais ameshauriwa kuachana na suala la kuwalipia makocha wa timu za taifa kama ambavyo amekuwa akifanya Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Badala yake, Magufuli ameshauriwa, iwapo atashinda na kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, basi atumie fedha hizo kukuza na kuendeleza vipaji vya soka na michezo mingine. Vipaji ambavyo baadaye vitakuwa msaada kwa maendeleo ya michezo nchini kwa jumla.
Hayo yametolewa na mchambuzi maarufu wa soka Tanzania anayeandikia gazeti hili, Saleh Ally, kupitia uchambuzi wake wa Metodo ambao unapatikana katika Ukurasa wa 20 wa gazeti hili, unaweza kuusoma zaidi katika ukurasa huo.

No comments:
Post a Comment