Sweetbert Lukonge na Nicodemus Jonas
SIKU moja tu baada ya kuibuka na ushindi wa kishindo na kupata nafasi ya mgombea wa urais kupitia chama kikongwe nchini cha CCM, Dk John Pombe Magufuli, tayari ameshauriwa mambo kadhaa kama moja ya mizigo anayotakiwa kuipatia ufumbuzi akishinda kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Magufuli alipata kura 2,104 ambazo ni 87% ya kura 2,422 zilizopigwa na kuwa ni dalili nzuri kwamba hata kwenye uchaguzi mkuu Oktoba atafanya vema.
Kitendo hicho cha urais kunukia kwake, kumeifanya klabu kongwe ya soka nchini, Yanga, kuwa ya kwanza kupitia Katibu Mkuu wake, Dk Jonas Tiboroha, kumpa Magufuli, mzigo wa kuufanyia kazi.
Lakini Simba na baadaye Azam FC ambazo ndizo klabu kubwa zinazochuana sasa katika kipindi hiki, nazo zikatoa yao kwa Magufuli.
Yanga:
Lakini Simba na baadaye Azam FC ambazo ndizo klabu kubwa zinazochuana sasa katika kipindi hiki, nazo zikatoa yao kwa Magufuli.
Yanga:
Akizungumza na Championi Jumatatu, Dk Tiboroha alisema furaha yake ni kusikia kupitishwa kwa mtu mpenda michezo tangu akiwa masomoni.
“Uzuri ninamfahamu vizuri, Magufuli ni mwanamichezo mwenzetu. Nilimfahamu tangu nikiwa masomoni pale chuoni (Chuo Kikuu Dar es Salaam-UDSM), kila siku alikuwa akifanya mazoezi ya kukimbia. Hivyo ni furaha kwetu kwa watu wa soka na anatakiwa kuanzia pale alipoishia Rais Kikwete,” alisema Dk Tiboroha.
“Akishinda, tunaomba serikali yake itambue kuwa changamoto kubwa kwenye soka letu ni suala la udhamini. Hivyo iwe tayari kushawishi makampuni makubwa ili yawekeze kwenye soka letu.
“Ligi kubwa zote zimeendelea kutokana na kuwa na udhamini mkubwa na wa kutosha, hivyo ili na sisi tuweze kufanya vizuri lazima tupate udhamini.
“Ligi kubwa zote zimeendelea kutokana na kuwa na udhamini mkubwa na wa kutosha, hivyo ili na sisi tuweze kufanya vizuri lazima tupate udhamini.
“Lakini pia ni lazima atambue kuwa soka kwa sasa ni ajira hususan kwa vijana, hivyo ni lazima sekta hii ipewe kipaumbele kama moja ya sekta ya kutoa ajira kwa vijana,” aliongeza Dk Tiboroha.
Simba:
Simba:
Kwa upande wa Simba, Makamu wa Rais, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amesema kuwa uteuzi huo wa Magufuli una faida kubwa katika medani ya soka.
“Mimi ni CCM damu, lakini nawapongeza sana CCM kwa hatua hiyo ya kumteua Magufuli kuwa mgombea wa nafasi ya urais wa nchi yetu, hakika hawajakosea kumpatia nafasi hiyo.
“Akifanikiwa kushinda aangalie mambo yafuatayo kwa ajili maendeleo ya michezo hapa nchini, hususan soka kwani tumechoka kuwa wasindikizaji kila wakati.

“Kwa kushirikiana na TFF, serikali yake iwe na mipango madhubuti ya kutengeneza wachezaji kuanzia ngazi ya chini kabisa kama yafanyavyo mataifa mengine.
“Lakini pia anatakiwa kuhakikisha kunakuwa na uwekezaji wa hali ya juu kwa kuwa na miundo mbinu mizuri ya mchezo, ukiangalia kwa asilimia kubwa viwanja vingi hapa nchini siyo vizuri, ni vibovu, hivyo ni matumaini yangu kuwa hilo ataliangalia.
“Mbali na hayo, pia timu za taifa anatakiwa kuziangalia kwa jicho la pekee, vizuri atenge bajeti kwa timu hizo, pia klabu zinazowakilisha Tanzania kimataifa.”
Azam FC:
“Mbali na hayo, pia timu za taifa anatakiwa kuziangalia kwa jicho la pekee, vizuri atenge bajeti kwa timu hizo, pia klabu zinazowakilisha Tanzania kimataifa.”
Azam FC:
Naye, Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, amesema: “Vipo vingi vya kuboresha lakini aanze na suala la viwanja vya soka, vipo vingi ambavyo vinamilikiwa na CCM na serikali lakini havitumiki ipasavyo au vimesahaulika kwa hiyo ni vema kwanza vikaanza kuboreshwa hasa sehemu za kuchezea ‘pitch’.
“Anatakiwa pia kuhimiza na kuangalia makampuni makubwa yanayoweza kuwekeza kwenye soka kwa ajili ya kufika mbali kupitia kwa watu hao wenye uwezo mkubwa wa udhamini.
“Kingine ni kuhusu kuthaminika kwa wachezaji wetu, kwanza ieleweke kuwa soka ni ajira na iwekewe mkazo ikiwemo hata kima cha chini cha mshahara wa mchezaji kiwe wazi na itambulike ni ajira kama nyingine.”

No comments:
Post a Comment