Diamond Platinumz akifanya yake katika red carpet ya tuzo za MTV.
Musa Mateja
KIWANGO! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia staa mkubwa duniani, Shaffer Chimere Smith ‘Ne-yo’ kuukubali uwezo wa kimuziki alionao kijana kutoka Tandale, Dar es Salaam, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Ijumaa Wikienda linakupa mchapo kamili.
Kabla ya Mmarekani huyo aliyewahi kutamba na Wimbo wa Miss Independent kuukubali uwezo wa Diamond, mastaa mbalimbali wa Afrika wakiwamo David Adedeji Adeleke ‘Davido’ na P-Square (Peter na Paul Okoye) wa Nigeria, kwa nyakati tofauti waliwahi kuripotiwa kwenye vyombo vya habari wakiguswa na uwezo wake na kuamua kufanya naye kolabo.
Mtangazaji wa Clouds FM, Hamis Mandi aka B-12 aka B-Dozen akiwa katika pozi na Diamond.
TUJIUNGE SAUZ
Kwa mujibu wa chanzo makini kilichoripoti ‘live’ kutoka Durban, Afrika Kusini (Sauz), wikiendi iliyopita kulikofanyika Tuzo za MTV Africa Music (Mama), Ne-yo ndiye aliyekuwa wa kwanza kuonesha shauku ya kutaka kumjua Diamond.
“Jamaa (Ne-yo) yeye mwenyewe ndiye aliyeonesha kuwa na shauku kubwa ya kutaka kumuona Diamond kwa sababu tayari alikuwa anafahamu habari zake na muziki wake.
AMSAKA HOTELINI
“Alilazimika kuanza kumsaka kwenye hoteli aliyofikia Diamond na kubahatika kukutana na meneja wa staa huyo aitwaye Salam. Akaomba amuitie Diamond kwani amekuwa akimfuatilia kwa muda mrefu katika mitandao mbalimbali ya kijamii,” kilisema chanzo hicho.
Wakipongezana.
MENEJA ATEKELEZA FASTA
Kikizidi kumwaga ‘ubuyu’, chanzo hicho kilisema, baada ya Salam kuombwa amuite Diamond, alimuongoza Ne-yo moja kwa moja hadi kwenye moja ya studio iliyopo jirani na hoteli waliyofikia jijini humo na kumkutanisha naye.
WAPEANA ‘HI!’
Kilisema kuwa, baada ya kufika, walisalimiana ambapo Ne-yo alionekana kwa asilimia kubwa kumkubali Diamond kwani baada ya kumuona alimwambia wazi kuwa amekuwa akimsikia mara kadhaa na kufuatilia kazi zake, hivyo siku hiyo alitamani kumuona kabla ya kutumbuiza kwenye hafla ya tuzo hizo.
“Waliongea mambo kibao huku wakipiga picha kisha Ne-yo akapiga picha na kruu nzima ya Wasafi Classic Baby (WCB) na kuondoka na Diamond hivyo kilichoendelea huko sikujua ni nini lakini kama unavyomjua mtoto wa Tandale kwa kutumia fursa, lolote linaweza kutokea,” kilisema chanzo hicho.
DIAMOND AFUNGUKA
Paparazi wetu, baada ya kumwagiwa ubuyu huo, alimtafuta moja kwa moja Diamond kupitia ‘kiLongaLonga’ chake ili aweke wazi kama kuna ‘project’ yoyote itakayofanyika baada ya kukutana na Ne-yo.
“Nilikuwa zangu sehemu naongea na D-Banj (staa wa Nigeria), meneja wangu (Salam) akaja akaniambia Ne-yo amenifuata hivyo tukakutane naye, akaniambia kuwa amekuwa akisikia Diamond, Diamond, Diamond lakini hatimaye ameniona na amefurahi.
“Jamaa ananikubali mno. Kama hiyo haitoshi jana (Alhamisi iliyopita) alikuwa akihojiwa na Vanessa Mdee, alipoulizwa ni mwanamuziki gani anamkubali sana Afrika akasema ni mimi.
WATAFANYA KOLABO?
“Kuna mambo mengi sana ya msingi tumeongea naye hivyo kwa sasa siwezi kuyaweka wazi lakini kama unavyonijua mwanao huwa sina muda wa kupoteza, nikikutana na watu kama hawa lazima nitumie nafasi yangu bila kuzubaa,” alisema Diamond huku akishiria kuwa kuna kitu tayari wameshapanga kufanya na Ne-yo.
Akiwa na Peter wa P – Square.
DIAMOND APIGA SHOO YA NGUVU
Mbali na kuwania tuzo hizo za MTV Africa Music (Mama), usiku wa Jumamosi iliyopita Diamond alipiga bonge la shoo katika hafla ya tuzo hizo sambamba na Ne-yo na Davido. Diamond Platnumz ametwaa tuzo ya MTV ya Best Live Act na kuwamwaga wasanii Mi Casa -South Africa, Flavour- Nigeria, Big Nuz -South Africa naToofan- Togo.
…Akiwa amelala baada ya kushinda tuzo hiyo.
NE-YO NI NANI?
Ne-yo mwenye umri wa miaka 35 ni staa mkubwa wa muziki wa RnB duniani aliyewahi kufanya kazi na lebo yenye umaarufu mkubwa Marekani ya Def Jam Recordings inayomilikiwa na rapa Jay-Z
Mbali na kuwa mwanamuziki mkali, Ne-yo ambaye pia ni prodyuza na muigizaji, ameshawaandikia mashairi wasanii wengi maarufu duniani akiwemo Mario (Let Me Love You) wimbo ambao ulikamata namba moja katika chati za Billboard Hot 100.
No comments:
Post a Comment