EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, July 7, 2015

SAA 48 ZA ANAKATWA, HAKATWI

MAKONGORO OGING NA OJUKU ABRAHAM
WAKATI jina la waziri mkuu wa zamani, Edward Ngoyai Lowassa likitajwa kila kona katika kinyang’anyiro cha kusaka nafasi ya kuwania urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), saa 48 zimesalia kufahamu kuwa jina la mgombea huyo litakatwa au halitakatwa katika mchujo wa kwanza, Uwazi linashuka nayo.
Waziri mkuu wa zamani, Edward Ngoyai Lowassa.
Duru za kisiasa nchini zinauangazia mkutano unaowahusisha wajumbe 32  wa Kamati Kuu (CC) ya chama hicho utakaofanyika keshokutwa (Alhamisi) kuwa ndiyo utakaotegua kitendawili cha wagombea gani watapenya kwenye hatua ya Tano Bora na majina yao kupelekwa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) kwa ajili ya kupigiwa kura ya awamu ya pili.
ITAKAVYOKUWA
Muongozo wa kumpata mwakilishi wa nafasi ya urais kupitia CCM unaonesha kuwa, majina ya wagombea watano yatakayopitishwa na CC yatachekechwa tena na Nec na kuwapata wagombea watatu ambao watakwenda kupigiwa kura na wajumbe wa Mkutano Mkuu  ambapo mshindi mmoja atapatikana na kukiwakilisha chama kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu.
ANAKATWA, HAKATWI YA LOWASSA INATOKA WAPI?
Pamoja na kuwa ndiye mgombea anayeonekana ana nguvu kwa kuungwa mkono ndani na nje ya chama chake, Lowassa amekuwa katika msukosuko mkubwa wa kisiasa kutoka kwa mahasimu wake ambao wamekuwa wakifanya kila linalowezekana kuhakikisha kwamba mwanasiasa huyo hapewi nafasi ya urais.

Mwenyekiti wa CCM,  D.r Kikwete makamu mwenyekiti Philip Mangula (katikati) na waziri mkuu Mizengo Punda wakifuatilia jambo.
Tuhuma ambazo wamekuwa wakimhusisha nazo ni pamoja na ufisadi, matumizi ya fedha katika kutafuta uungwaji mkono na uanzaji kampeni mapema, mambo ambayo yamewekewa zuio na CCM na hivyo kuwafanya wanaomjengea hoja za kukataliwa kushikilia silaha hiyo kwa lengo la kumdhoofisha matumaini ya kupitishwa na vikao vya chama.
Hata hivyo, wanaomuunga mkono pamoja na Lowassa mwenyewe wamekuwa akipuuza madai hayo huku wakiwataka wanaoshabikia mambo hayo kuweka ushahidi wa kutosha juu ya madai yao, la sivyo waache kufanya siasa za maji taka.

“Nimekuwa mwana CCM tangu mwaka 1977 nilipomaliza chuo kikuu, sijawahi kufanya kazi nje ya CCM. Hivyo nakijua chama na hakuna mgombea atakayeweza kuvunja rekodi ya utendaji wangu katika chama. Sasa leo anayetaka kukata jina langu anatoka wapi? Anakata kwa sababu gani?
Kinana.
“Sioni kosa la kukatwa jina na Watanzania hawaoni. Kwa hiyo msiwe na wasiwasi jina litarudi tu,” Lowassa aliwaambia maelfu ya watu waliojitokeza kumdhamini alipowasili mkoani Ruvuma hivi karibuni.
AKIKATWA ITAKUWAJE?
Mmoja kati ya wafuasi wa Lowassa, ambaye amekuwa akijipambanua pia kuwa ni msemaji wake, Hussein Bashe  amewahi kunukuliwa akisema: “Kama CCM watamkata Lowassa kwa hila watarajie kukutana na nguvu za umma.”
Ingawa Bashe hakufafanua zaidi nguvu ya umma itafanya nini na kwamba mgombea wao atafanyaje jina lake likiondolewa lakini duru za kisiasa zinaonesha kuwa huenda chama hicho kikapata mtikisiko mkubwa kutokana na kile kinachotajwa kuwa  ni Lowassa kuwa na mtaji mkubwa wa watu wanaomuunga mkono.
Katika safari yake ya kusaka wadhamini, mgombea huyo amekuwa akitikisa kwa kupata mapokezi makubwa karibu katika kila mkoa aliyokwenda ambapo ameweza kujikusanyia zaidi ya wadhamini laki nane, ingawa wanaohitajika na chama ni 450 tu kutoka katika mikoa 15.
Dr. Shein
CHAMA KIKOJE?
Kama ilivyo kwa jina lake kuondolewa, Lowassa bado anakiweka njia panda chama chake kutokana na kuwepo kwa makundi ndani ya chama hicho ambayo yanaonesha kuwa hayako tayari kumuunga mkono katika safari yake ya kuingia ikulu.
Yeye waziri mkuu wa zamani, Fredrick Sumaye ameshatangaza mgogoro na chama chake endapo jina lake litaondolewa na kwamba yuko tayari kukihama chama hicho kama dalili za kuwapendelea anaowaita mafisadi zinavyoonekana.
Philip Mangula
Hata kama wagombea nafasi ya urais ndani ya CCM wamekuwa wakishindwa kutaja moja kwa moja jina la Lowassa katika tuhuma zao za ufisadi, wachambuzi wa mambo wamekuwa wakitafsiri kuwa zinamwelekea waziri mkuu huyo wa zamani aliyejiuzulu kwa tuhuma za ufisadi uliosababishwa na ugawaji wa tenda ya Taasisi ya Kufua Umeme ya Richmond uliofanywa kinyume cha sheria miaka ya 2000.
Mtazamo huu, huenda ukaathiri umoja wa CCM tofauti na miaka ya nyuma endapo chama kitaamua kumpitisha mgombea ambaye wenzake wanamchukulia kama mtu asiyefaa kupewa nafasi hiyo, mwenyekiti wa chama na amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama.
SAA 48 ZIKO KWA HAWA
Pamoja na mitazamo yote, wajumbe wa kamati kuu ambao macho na masikio ya wengi yanawatazama na kusikia uamuzi wao kesho kutwa ni hawa wafuatao:
Nape Nnauye
Jakaya Kikwete (mwenyekiti), Dk. Alli Mohamed Shein, Phillip Mangula, Abdulrahman Kinana (katibu), Dk. Mohamed Ghalib Bilal, Mizengo Pinda, Balozi Seif Ali Idd, Anna Makinda, Pandu Amir Kificho, Vuai Ali Vuai, Rajab Luhwavi na Nape Nnauye.
Wengine ni Mohammed Seif Khatib, Zakhia Hamdan Meghji, Asharose Migiro, Sofia Simba, Sadifa Juma Khamis, Abdallah Majura Bulembo, Jenista Mhagama, William Lukuvi, Pindi Chana, Jerry Silaa, Adam Kimbisa, Shamsi Vuai Nahodha na Hussein Mwinyi.
Mbali na wajumbe hao, wapo pia Maua Daftari, Samia Suluhu, Salim Ahmed Salim, Makame Mbarawa na Hadija Abood. Hata hivyo, katika kikao cha kuchuja majina hayo,  wagombea waliotangaza nia hawataruhusiwa kuingia kwenye uteuzi wa majina.

CHANZO: UWAZI

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate