KIONGOZI Mkuu wa Chama Cha ACT – Wazalendo, Zitto Zuber Kabwe jana amewaacha njia panda wananchi waliokuwa wakisubiria kutaja orodha ya majina ya watu wanaotuhumiwa kuwa na akaunti zenye mabilioni ya fedha nje ya nchi, baada ya kusita kuyataja kutokana na sababu za kisheria.
Akizungumza na umati mkubwa uliofurika katika viwanja hivyo jana jijini Dar es Salaam, kusikiliza azima ya kiongozi huyo huku wakiwa na shauku kubwa ya kufahamu orodha ya majina hayo, Zitto alisema kuwa atawapatia karatasi waandishi wa habari yenye orodha ya majina hayo ili waende kuifanyia kazi kwa kuwahoji wahusika kulingana na taaluma yao.
Alisema kuwa mwisho wa hotuba yake angegawa karatasi kwa wanahabari yenye majina hayo, ambapo wananchi walionekana kuwa na shauku ya kupata karatasi hiyo yenye majina 99 ya wafanya biashara maarufu ndani na nje ya nchi, lakini Zitto akasema hakuwa tayari kuwapatia nakala hiyo wananchi, hivyo akawataka wafuatilie katika mitandao ya kijamii pamoja na kwenye vyombo vya habari kwani wao kwa kutumia taaluma yao wanao uhuru wa kuyaanika hadharani.
Aidha, aliongeza kuwa kati ya majina hayo ya watu wenye mabilioni ya fedha nchini Uswisi, kuna wengine wanamiliki kihalali lakini wengine wamejilimbikizia kinyume cha sheria.
“Nimeweka leo orodha ya majina hayo wazi ili kuiwezesha serikali kutoa taarifa ya uchunguzi kabla ya Bunge kuvunjwa wiki ijayo, majina 99 mtayapata kupitia kwa wanahabari niliowapatia nakala yenye orodha ya vigogo hao ama Watanzania walio na akaunti kwenye HSBC ya Uswisi ikiwa na akiba ya Dola 114 milioni za Marekani,” alisema Zitto.
Baada ya kuhitimisha mkutano hao, kiongozi huyo wa ACT aligawa karatasi hiyo kwa baadhi ya waandishi wa habari.
IFUATAYO NI ORODHA YA MAJINA HAYO:
Comment
- Comment by simba nylon 19 hours ago
-
Delete Comment
Kama alikuwa anajua mambo ya sheria kwann aliahidi kuyaweka hadharani?
Na kama wengine wanamiliki kihalali wanahusiana vp na wizi na ufisadi
Huoni kuwa Ni kuingilia mambo binafsi ya watu mambo yay fedha Ni faragha
Acha kutafuta cheap popularity
- Top News
- Everything
Ahh thanks for this i appreciate your candor
ReplyDelete