Mayasa mariwata na Shani ramadhani
HATARI! Kufuatia kuwepo kwa madai kwamba, baadhi ya wakaanga chipsi mijini, hususan jijini Dar, wamekuwa wakitumia mafuta ya transifoma kukaangia chakula hicho, timu ya Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ya Global Publishers iliingia mtaani kwa lengo la kujiridhisha.
OFM iliingia kwenye viunga mbalimbali vya jiji hasa sehemu ambazo zina vibanda vya wauza chipsi na kuzungumza nao.
Muuza chipsi maeneo ya Mwananyamala aliyejitambulisha kwa jina moja la Ushie, alipoulizwa kuhusu kuwepo kwa madai hayo, alisema amesikia wapo wanaotumia lakini yeye hatumii.
Mwingine alikutwa na OFM maeneo ya Kinondoni akajitambulisha kwa jina la Idi Juma. Yeye alisema: “Kuna mtu aliwahi kuniletea mafuta ya transifoma akidhani nitanunua ili niwe natumia kukaangia chipsi nikagoma. Lakini wapo wauza chipsi wengi ambao si waaminifu wanatumia.”
Karibu wauza chipsi wote walioulizwa na OFM hawakukiri kuhusu kutumia mafuta hayo. Lakini walisema wenzao wanatumia.Inadaiwa kuwa, wauzaji wanapenda mafuta ya transifoma kwa sababu yanaweza kutumika kwa muda mrefu, hata mwezi mmoja bila kukauka kwenye karai na hayafanyi chipsi kuwa nyeusi kama mafuta halali. Inadaiwa pia, chipsi zilizokaangwa na mafuta hayo ni tamu sana.
Jumatano iliyopita, OFM ilizungumza na Afisa Habari wa Shirika la Ugavi Tanzania (Tanesco), Adrian Severin na kumuuliza kama shirika linajua kutumika kwa mafuta hayo kukaangia chipsi ambapo alisema:
“Tunajua japokuwa hatujawahi kuthibitisha kwa kumwona mtu akiyatumia. Wengine wanayatumia kwenye vipodozi, wengine wanachanganya na oil ya magari. Lakini Tanesco tunatoa wito kwa Watanzania, hususan wanaoishi jirani na transifoma kutoa taarifa mara wanapomwona mtu anapanda kwenye transifoma huku si mfanyakazi wa Tanesco.
“Wizi wa mafuta haya unasababisha transfoma kushindwa kufanya kazi na hivyo maeneo husika kukosa umeme.”
“Wizi wa mafuta haya unasababisha transfoma kushindwa kufanya kazi na hivyo maeneo husika kukosa umeme.”
OFM lilimtafuta daktari mmoja wa jijini Dar es Salaam, dokta Chale kwa lengo la kumuuliza kama mafuta ya transifoma yakitumika kwenye chakula yana madhara, akajibu:
“Makubwa tu. Kwanza, mtumiaji anaweza kupata ugonjwa wa kansa ya tumbo. Pili, hayo mafuta yanaweza kusababisha maini na figo kushindwa kufanya kazi. Na tabia hii ikiendelea, Wabongo wengi watakufa.”
CHANZO: Global Publishers
No comments:
Post a Comment