Mwenyekiti wa Bodi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Norman Sigara Aikzungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu kufukuzwa kazi kwa madaktari hao |
Mkurugenzi wa wa hospitali ya rufaa Mbeya Dr E. Sankey akimsikiliza kwa makini kaimu mkuu wa mkoa Mbeya
|
BODI
ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya, imewasimamisha kazi madaktari
72 kwa kosa la kutoingia kazini kwa siku tano jambo ambalo ni kinyume
cha makubaliano ya mkataba.
Imeelezwa
kuwa madaktari hao ambao 54 ni wale wa mafunzo ambao waliingia mkataba
wa miaka miwili na hospitali ya Rufaa na madaktari 18 ni wale
walioajiriwa na Wizara ya afya.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Bodi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya
Norman Sigara, alisema kitendo cha madaktari kutoripoti kazini kwa siku
tano ni ukiukwaji wa kanuni za utumisha wa umma toleo la 2009 kifungu
namba F.16-F17 na F. 27.
"Hivyo
kupitia kanuni hiyo madaktari hao wamesimamishwa kazi na kurudishwa kwa
mwajiri wao ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa
hatua zaidi za kinidhamu,"alisema Sigara.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti huyo wa Bodi, imeelezwa kuwa siku ya tarehe
23/6/2012 wafanyakazi 15 waliokuwa zamu(Intern Doctors 12 na
Registrars3) hawakufika kazini na tarehe 24/6/2012 wafanyakazi 19(Intern
doctors 15 na Registrars 4) hawakufika kazini.
Alisema,
kuanzia tarehe 25/6/2012 hadi leo imethibitika kuwa Interns doctor 54
na Registrars 18 hawakufika kazini hadi leo tarehe 28/6/2012 ambapo
tarehe 25/6/2012 bodi ya hospitali ilifanya kikao cha dharura kujadili
hali ya utendaji kazi na utoaji huduma hospitalini na kutoa uamuzi.
Sigara,
aliyataja maamuzi hayo kuwa ni Mwenyekiti wa Bodi akutane na madaktari
ambao hawakufika kazini ili awasikilize sababu za kutofika na kujadili
namna ya kumaliza matatizo hayo jambo ambalo madaktari hao waligoma.
Alisema,
baada ya madaktari hao kukaidi ombi hilo, Bodi ya hospitali ili
waandikia barua za kujieleza kwanini wasichukuliwe hatua za kinidhamu
kwa kuvunja mkataba walioingia na hospitali na pia kukiuka kanuni za
kudumu za utumishi wa umma nalo walilikaidi
"Iwapo
madaktari ambao hawakuripoti au kueleza sababu za kuridhisha ifikapo
tarehe 28/6/2012. Kwa kuzingatia kanuni za utumishi wa Umma, madaktari
hao watasimamishwa kazi na kurudishwa kwa mwajiri wao ambaye ni Katibu
Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,"alisema.
Aidha,
alisema kuwa kwa ujumala madaktari hao waligomea barua zote mbili yaani
ya kuitwa kwenye kikao pamoja na ile ya kuwataka kujieleza hivyo Bodi
imechukua hatua za kisheria za kuwafukuza kazi.
Hata
hivyo Mwenyekiti huyo wa bodi, alisema kuwa tayari hospitali ya Rufaa
kwa ushirikiano wa Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, madaktari watano
wamepatikana ili kusaidia huduma kwa hospitali hiyo.
CHANZO CHA HABARI MBEYA YETU BLOG
No comments:
Post a Comment