Muandaaji wa Tamasha la Filamu la TOFF, Musa
Kissoky (katikati) akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam jana. Wengine pichani ni Meneja wa Masoko wa
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Fimbo Butala (kushoto) na nyota wa Bongo
Muvies, Vicent Kigosi a.k.a Ray
Nyota mbalimbali
wa filamu nchini, akiwemo Wema Sepetu, Jacqueline Wolper, Irene Uwoya na
Vicent Kigosi 'Ray' kwa mara ya kwanza watapanda kwenye jukwaa moja la
tamasha la filamu litakalofanyika jijini Tanga kuanzia keshokutwa
Jumamosi hadi Julai 6 mwaka huu.
Mratibu wa tamasha hilo, Mussa Kisoky wa Sophia Records, alisema kuwa katika tamasha hilo kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wa Tanga wanaoimba ngoma za asili kama baikoko, mdumange na msanga.
Kisoky alisema vilevile kuwa wakiwa Tanga, wasanii hao watatembelea Hospitali ya Mkoa ya Bombo na kutoa misaada ya vyandarua kwa wodi ya wazazi na watoto ili kuwakinga na ugonjwa wa malaria.
Alikitaja pia kikundi cha taarab cha Tanzania Moto kinachoundwa na wanamuziki waliong'ara East African Melody na Zanzibar Star kuwa watasindikiza tamasha hilo.
Mbali na akina Wema, wasanii wengine waliothibitisha kushiriki ni Jacky Pentezel 'Jacky wa Chuz', Aunt Ezekiel, Rich Rich, Sandra, Steve Nyerere, Chick Mchoma, Jacob Steven 'JB' na Issa Mussa 'Cloud'.
Akizungumza jana, Meneja wa kinywaji cha Grand Malt ambao wanadhamini tamasha hilo, Consolatha Adam, alisema Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), imetumia zaidi ya Sh. milioni 90 ili kuandaa tamasha hilo ambalo lengo lake ni kuwakutanisha wadau wa filamu na mashabiki wao.
Alisema kuwa kupitia tamasha hilo wananchi watahamasishwa zaidi kupenda kazi za wasanii wa nchini na vile vile wasanii hao watabadilishana mawazo na mashabiki wao.
"Lengo letu ni kulikuza tamasha hili ambalo linafanyika kwa mwaka wa nne na tunaamini itakuwa ni faraja kwa wadau wa sanaa kukutana na wasanii wanaowaona ana kwa ana na kujifunza kupitia kazi zao," alisema Consolatha.
Mwenyekiti wa Bongo Movie, JB, alisema kuwa wanawashukuru waandaaji wa tamasha hilo na kwamba, wanatarajia kuteua wasanii watatu chipukizi watakaofanya nao kazi.

CHANZO: GAZETI LA NIPASHE
No comments:
Post a Comment