Italia ilipata ushindi dhidi ya
timu ya Jamhuri ya Ireland ambayo tayari wachezaji wake walikuwa
wanajitayarisha kuondoka kutoka mashindano ya Euro 2012, kwa kuwafunga
magoli 2-0.
Jamhuri ya Ireland walianza mchezo huo wa Jumatatu usiku, wakithibitisha nia yao ya kujitahidi kupata ushindi, lakin ni Antonio Cassano, mchezaji wa Italia, ndiye aliyefanikiwa kuliona lango kwanza, akitumia kichwa, kufuatia mpira wa kona iliyopigwa na Andrea Pirlo.
Iwapo Ireland ingelisawazisha, kama alivyokaribia kufunga Keith Andrews lakini kipa wa Italia Gianluigi
Buffon akaweza kuokoa, ingelimaanisha Italia, katika kundi C, wangelijikuta wametupwa nje ya mashindano hayo ya Ulaya, hasa kama Croatia ingelipata bao la kusawazisha dhidi ya Uhispania, mechi iliyochezwa sambamba na hii, na iliyokwisha kwa ushindi wa Italia wa bao 1-0.
Andrews aliamrishwa na mwamuzi kuondoka uwanjani, baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya manjano, na Mario Balotelli akafanikiwa kufunga bao la pili na kuwatuliza mashabiki wa Italia.Kutokana na Uhispania kuishinda Croatia, sasa itakutana na mshindi wa kundi D.
England ni miongoni mwa mataifa katika kundi hilo.
----------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Mabingwa watetezi waingia robo fainali
Jesus Navas alikuwa ni mkombozi
wa timu ya hispania, kupitia bao la dakika za mwishomwisho dhidi ya
Croatia, na kuiwezesha nchi yake kufuzu kuingia robo fainali katika
mashindano ya Euro 2012.
Ilielekea kana kwamba mabingwa watetezi Uhispania walikuwa wakicheza mechi hiyo ya Jumatatu usiku kwa wasiwasi.
Hata
hivyo Jesus, ambaye ni mchezaji wa Seville ya hispania, aliweza
kuupokea mpira uliopigwa kwa maarifa na Andres Iniesta, na zikiwa
zimesalia dakika mbili kabla ya mechi kumalizika, kuiandikishia hispania bao, na kuwahuzunisha mashabiki wa Croatia.
Bao hilo moja lilihakikisha hispania inaongoza kundi la C.
hispania walicheza karata yao vyema, kwani kwa
kumtoa Fernando Torres na mahala pake kuingia Jesus Navas, ni mchezaji
huyo wa zamu aliyeweza kufunga bao.
Sasa mabingwa watetezi wanasubiri kujua kama
watakutana na England au Ufaransa katika timu nane ambazo zitasalia
kucheza robo fainali.
Chanzo cha habari BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment