Ni
dhahiri mgomo sasa hauepukiki keshokutwa, baada ya kile kinachodaiwa
kushindwa kwa serikali kutoa majibu ya utekelezaji wa madai mbalimbali
ya madaktari nchini.
Hali hiyo imedhihirika kufuatia
madaktari katika hospitali mbalimbali nchini kujitokeza hadharani na
kutangaza azma yao ya kugoma keshokutwa kuishinikiza serikali kutekeleza
madai yao.
Wasiwasi wa kufanyika mgomo huo
unakolezwa na kimya cha serikali ambayo licha ya madaktari hao kutangaza
azma yao ya kugoma, hadi kufikia jana serikali ilikuwa bado haijatoa
taarifa yoyote kuhusiana na hatima ya utekelezaji wa madai ya madaktari.
Akizungumza na NIPASHE jana jijini
Dar es Salaam, Kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Steven Ulimboka,
alisema kufikia jana walikuwa hawajapokea taaraifa yoyote kutoka
serikalini kuhusiana na madai yao.
Dk. Ulimboka
Dk. Ulimboka alisema kuwa leo wanatarajia kutoa tamko kuhusiana na suala hilo.
Dk. Ulimboka
Dk. Ulimboka alisema kuwa leo wanatarajia kutoa tamko kuhusiana na suala hilo.
Wakati madaktari wakijianda kugoma,
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi, amesema kuwa
serikali inasubiri maamuzi ya Tume ya Usuluhishi kwa kuwa suala hilo
liko katika mkondo wa sheria.
Akizungumza na NIPASHE jana jioni,
Dk. Mwinyi alisema serikali haiwezi kulizungumzia suala hilo kwa kuwa
inasubiri sheria ifuate mkondo wake.
Alisema wakati wa mgomo wa kwanza,
suala hilo lilifikishwa mahakamani na mahakama kuamua liende katika Tume
ya Usuluhishi ambayo ilitoa muda kwa serikali na madaktari kujadiliana
ili kufikia mwafaka.
Alisema juzi Tume hiyo ilitakiwa
kufuatilia makubaliano, lakini madaktari walikwenda katika Tume na
kusema kuwa hawajakubaliana na serikali.
Hata hivyo, alisema kati ya madai
10 ya madaktari, matano yamekelezwa. Moja ya madai hayo alisema ni
kuongezwa kwa posho ya kuitwa kazini kutoka Sh. 10,000 hadi Sh. 25,000.
Posho nyingine ni posho ya
uchunguzi wa maiti kutoka Sh. 10,000 hadi Sh. 100,000 kwa daktari bingwa
na wasaidizi wake Sh. 50,000. Nyingine ni kupewa kadi ya kijani kwa
ajili ya huduma za afya na kupewa chanjo ya kujikinga na magonjwa ya
kuambukiza.
Dk. Mwinyi alisema dai lingine la kutaka uongozi wa wizara kubadilishwa limeshatekelezwa.
Hivi karibuni, madaktari waliipa
serikali wiki mbili kuhakikisha inatekeleza madai yao, vinginevyo
watagoma tena kama mgomo wa Januari na Fenruari mwaka huu uliotikisa
sekta ya afya na kusababisha madhara makubwa kwa wagonjwa katika
hospitali nyingi za umma.
Pia hawakukubaliana na maelezo ya ripoti ya kamati ya serikali iliyopewa kazi ya kushughulikia madai ya madaktari.
Walisema ripoti hiyo imeshindwa kueleza jinsi madai yao yatakavyoshughulikiwa, likiwamo la nyongeza ya mshahara, ambapo walitaka kima cha chini kiwe Sh. milion 3.5.
Walisema ripoti hiyo imeshindwa kueleza jinsi madai yao yatakavyoshughulikiwa, likiwamo la nyongeza ya mshahara, ambapo walitaka kima cha chini kiwe Sh. milion 3.5.
Walidai wamegundua katika ripoti
hiyo kuwa serikali haina nia ya kutekeleza madai yao na kwamba kila
wanapokutana katika kikao, wamekuwa wakijibiwa majibu yasiyoridhisha.
Walisema kuna madai yao, ambayo
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, aliyatolea maamuzi walipokutana katika
mkutano uliowakutanisha madaktari wote katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MNH), ambayo kamati hiyo imeyaondoa wakati yalishafanyiwa
kazi.
Walisema Pinda aliwaambia katika
kipindi cha bajeti ijayo kuhusiana na posho ya madaktari kwa wale
wanaoitwa kuendelea na kazi wakati wanapokuwa katika mapunziko
walijulishwa kuwa daktari bingwa atapatiwa Sh. 50,000 na kwa daktari wa
kawaida atapatiwa Sh. 40,000. Hata hivyo, walisema suala hilo
limeondolewa.
Madaktari hao walisema katika suala
hilo kamati imeamua kuondoa utekelezaji huo na kubakiza Sh. 20,000 na
Sh. 25,000 kwa daktari bingwa, wakati Waziri Mkuu aliziongeza kwa
kiwango hicho na kuwaahidi kuwa katika bajeti ya mwaka 2012/2013
wataongezewa kiwango hicho.
Mbali na hayo, pia walisema kuna
mambo mbalimbali ambayo kamati hiyo imeshindwa kuwatekelezea licha ya
kwamba waliahidiwa kuwa yangefanyiwa kazi na serikali.
Kutokana na hilo, madaktari waliipa
serikali siku 14 kuhakikisha inatekeleza madai yao na kwamba kama
haitafanya hivyo wanajianda kufanya mgomo wa madaktari wote nchini.
Wakati Ulimboka akisema hivyo,
madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC mkoani Kilimanjaro jana
walitangaza kujiunga na mgomo huo iwapo serikali itashindwa kutoa majibu
ya madai yao.
Mwenyekiti wa madaktari hao, Dk.
Rosemary Mrina, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Juni 15, mwaka
huu, walikutana na kujadili kwa kina taarifa ya serikali ya kamati ya
majadiliano baina ya serikali na madaktari iliyoundwa wakati wa mgomo wa
awali.
Dk. Mrina alisema hawajaridhishwa na majibu ya serikali kwani yameshindwa kuwa na jibu la kutatua kero zao.
Kero hizo ni upungufu wa vifaa tiba na dawa, mazingira magumu ya kufanyia kazi, maslahi yao ikiwemo posho mbalimbali ambazo ni stahili zao.
Kero hizo ni upungufu wa vifaa tiba na dawa, mazingira magumu ya kufanyia kazi, maslahi yao ikiwemo posho mbalimbali ambazo ni stahili zao.
Daktari Mugisha Nkoronko ambaye ni
mjumbe wa kamati ya kitaifa ya kushughulikia madai ya madaktari alisema
tayari Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) kimetangaza mgogoro wa wiki
mbili kati yake na serikali, hivyo ni wazi kuwa watakaoathirika ni
wananchi.
“Hatupendi ile hali ya wakati ule
ijirudie, lakini serikali inatulazimu kufika huko kutokana na majibu
mapesi yaliyotolewa, tumepeleka madai ya kurasa 50 wamejibu kwenye
karatasi moja, moja ya maadui watatu tunaopigana nao tangu nchi ipate
uhuru ni maradhi, lakini serikali imeshindwa kutatua kero zetu ili nasi
tufanye kazi katika mazingira mazuri,” alisema.
Alisema madai ya madaktari
yamebebwa na hoja nzuri na za msingi, lakini majibu ya serikali ni
mepesi sana na ambayo huwezi kuyatarajia na kuwa mgogoro huo ulishafika
kwa rais ambaye aliingilia kati na kuahidi kuutatua, lakini hakuna
lililofanyika.
Dk. Anette Kessy alisema serikali
imewapuuza wakati mgogoro uliopita Rais Jakaya Kikwete aliahidi kuupatia
suluhu, lakini hadi sasa hakuna majibu waliyoyapata.
Juzi madaktari katika Hospitali ya Rufani ya Bugando jijini Mwanza walitangaza kuunga mkono mgomo huo.
CHANZO: NIPASHE
CHANZO: NIPASHE

No comments:
Post a Comment