MBUNGE wa Michewene, Haji Khatib Kai (CUF), jana aliihoji Serikali
akiitaka kutoa maelezo ya kina juu ya faida zinazopatiana kwa Watanzania
juu ya mwenge wa Uhuru.Kai alitoa kauli hiyo wakati akiuliza swali kwa
Waziri Mkuu katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo ambayo huulizwa
siku ya Alhamishi.
Mbunge huyo alisema katika kipindi kirefu amekuwa akishangazwa na kitendo cha Serikali kuendelea kupigia debe mbio za mwenge huku ikitambua kuwa unafanya kazi ya kuhamasisha mambo ya ngono katika mikusanyiko ya mikesha.
“Mheshimiwa Spika, mkesha wa mbio za mwenge mara nyingi huhamasisha masuala ya ngono ambayo hueneza Ukimwi na magonjwa mengine, je hamuoni kuwa jambo hilo ni kosa na halina faida kwa mustakabali wa nchi yetu,’’ alihoji Kai.Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema kuwa zipo faida nyingi katika mbio za mwenge Kitaifa na uwepo wake una umuhimu mkubwa zaidi kuliko inavyotazamiwa na wengi.
Pinda alisema kuwa kila Taifa duniani lina utaratibu wake katika kutengeneza mpango sahihi wa mambo ambayo hufanywa ili kusaidia kukumbuka mambo yao“Kwanza sio kweli kama mwenge unahamasisha mambo ya ngono, hapana, watu wanaweza kufanya mambo hayo wakati wowote, lakini kikubwa ni kwamba mwenge una faida kubwa zaidi na ninaomba ndugu zangu tuendelee kuamini na kuuheshimu,’’ alisema Pinda.

Alitolea mfano wa mbio za Olimpiki ambazo hukimbizwa
katika nchi mbalimbali kwa ajili ya kuhamasisha mambo kadhaa ikiwemo
amani na mshikamo.Waziri Mkuu alisema wazo la Mwenge liliasisiwa na
hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alipotaka kuweka chombo
ambacho kinaibua hisia za watu katika kukumbuka shughuli za kimaendeleo.Aliyataja
baadhi ya mafanikio kuwa ni pamoja na kuzindua miradi mbalimbali na
kuweka mawe ya msingi kwa maeneo tofauti kila wakati.
Kwa mujibu wa Pinda, kauli mbiu zinazotolewa katika mbio za mwenge huwafikia wananchi kwa urahisi zaidi kwani mbio hizo hukusanya idadi kubwa ya watu kwa mara moja.

Habari na Habel Chidawali,Dodoma
No comments:
Post a Comment