Msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael Kimemeta (18), maarufu kama
Lulu, anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba
(28), jana alirudishwa mahabusu bila kupanda kizimbani katika
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam hadi hapo Mahakama Kuu
Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, itakapotoa uamuzi kuhusu suala la
utata wa umri wake.
Baada ya mshtakiwa huyo kufikishwa mahakama hapo jana hakupandishwa kizimbani kutokana na jalada la kesi hiyo kuwa Mahakama Kuu, ambapo suala la utata wa umri wake litasikilizwa Juni 25, mwaka huu mbele ya Jaji

Dk. Fauz Twaib.
Lulu alirudishwa mahabusu kutokana na sheria kutoruhusu usikilizwaji wa awali kuendelea wakati Mahakama Kuu inaendelea kusikiliza maombi yaliyowasilishwa na mshtakiwa kutaka umri wake uchunguzwe.
Katika kesi hiyo, Lulu anatuhumiwa kumuua msanii mwenzake Steven Kanumba Aprili 7, mwaka huu katika eneo la Sinza Vatican jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment