MWANAMKE mmoja aliyefahamika kwa jina la Mama Mosha ambaye ni mfanyabiashara maarufu mjini Morogoro, jana mchana alinusurika na ajali baada ya gari alilokuwa akiendesha kutumbukia kwenye mtaro wa Barabara ya Korogwe eneo la Masika njia panda ya kueleka Fire.
Akizungumza na mtando huu mama huyo aliyekuwa akiendesha gari aina ya Suzuki yenye namba za ujasili T 515 ARQ, alisema chanzo cha ajali hiyo ni pale alipojaribu kumkwepa mpanda baiskeli aliyekuwa akitoka Barabara ya Fire na bila kuangalia akaingia barabara kuu.
Baada ya ajali hiyo, mpanda baiskeli huyo alikimbia.
(PICHA NA DUNSTAN SHEKIDELE, GPL / MOROGORO)
No comments:
Post a Comment