MKURUNGEZI
wa Kampuni ya Udalali ya Msama, Alex Msama akionesha siku ya janajijini Dar
es Salaam, CD zenye nyimbo za wasanii walizokamatwa nazo watu 8 baada ya
kudurufu kazi hizo za wasanii zenye dhamani ya milioni 25, Watuhumuwa
hao wapo katika Kituo cha Polisi Buguruni, Dar es Salaam.
Alex Msama akichambua cd hizo siku ya jana katika Kituo cha Polisi Buguruni, Dar es Salaam.
Msama akionesha cd hizo
Msama akizungumza na waandishi wa habari, kuhusu mkakati wa kuendelea kuwakamata watengenezaji na wauzaji wa CD hizo feki.
Baadhi ya CD zilizokamatwa
Majina ya watu 8 waliokamatwa wakiuza CD hizo. PICHA ZOTE NA KAMANDA MWAIKENDA
Na Asha Kigundula
MKURUNGENZI wa Kampuni ya Udalali ya Msama, Alex Msama akishirikiana na Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata watu 8 baada ya kudurufu kazi za wasanii zenye thamani ya sh.milioni 25.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Msama alisema wiki iliyopita walianza zoezi la kukamata watu wanaozidurufu kazi za wasanii mbalimbali ambazo wanauza kwa faida yao.
Msama alisema wakiwa maeneo ya Buguruni sheli, walifanikiwa kuzikamata kazi hizo zikiwa zinauzwa kwa bei ya chini.Alisema kuna baadhi ya kazi hata mtaani hazijaanza kutoka lakini wao wanazo na wakiuza kwa shilingi 1000 kila moja.
"Tumekuta kazi mbalimbali kama vile za muziki wa Injili, Movies, nyimbo za bendi muziki wa ndansi na taarab" alisema Msama.Alisema licha ya kukamata CD hizo za kusikiliza na kuonesha ilifanikiwa kukamata mashine moja ya kudurufu.
Msama alisema katika zoezi hilo waliwakamata watu nane wakiwa wanauza kazi hizo.Waliokamatwa ni Halfan Bakari, Hassan Bakari,Hemed Mohamed, Patrick Peter, Hashraf Rajab, Mkoya Peter na Khamis Athuman.
Msama alisema watuhumiwa hao wote wapo katika kituo cha Polisi Buruguruni kwa ajili ya uchunguzi.

No comments:
Post a Comment