EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, August 10, 2012

Ajali za bodaboda zaua 400

JESHI la Polisi kupitia kikosi cha Usalama barabarani  nchini kimesema  jumla ya ajali za pikipiki (bodaboda) 2601 zilizotokea kuanzia Januari hadi Juni mwaka huu zilisababisha vifo vya madereva  487 wa pikipiki hizo.

Akizungumza na gazeti hili jana ofisini kwake, Kamishna Msaidi wa Polisi, kikosi cha usalama barabarani Johansen Kahatano alisema ajali hizo zinazidi kuongezeka kila mwaka kutokana na sababu mbalimbali.

 “Kwa mwaka 2009 kulitokea ajali 3406 na waliokufa ni 502,mwaka uliofuata ajali 4363 na vifo 683 na ilipofikia mwaka 2011 zilitpkea ajali zingine 5384 na waliokufa ni 945, taarifa hii inaonyesha kuwa kila mwaka vifo vinaongezeka”alisema Kahatano.

Alisema kuongezeka kwa bodaboda na uelewa mdogo wa sheria za usalama barabarani kwa madereva hao ndiyo  sababu kubwa ya ongezeko la ajali hizo.

Alisema pikipiki zilizo sajiliwa mwaka 2009 kwa ajili ya biashara hiyo ni 87,826 na hadi kufikia mwaka 2011 kulikuwa na pikipiki  1,34,831 na kwamba wamiliki wake  wamekuwa hawana elimu ya kutosha kwa ajili ya kuwasaidia madereva wao.

Aliongeza kuwa kutokana na changamoto hiyo wamepata msaada kutoka kwa Taasisi zisizo za kiserikali kwa mikoa mbalimbali hapa nchini zinazotoa elimu ya mafunzo ya udereva kwa pikipiki ili kupunguza ongezeko la ajali

“Mafunzo hayo yalianza Juni mwaka huu,Kwa mkoa wa Tanga kuna taasisi  inayoitwa APEC inatoa mafunzo kwa Bodaboda 2000 hadi sasa na Mkoa wa Mtwara inaitwa British Gas inatoa mafunzo kwa Bodaboda 600,lengo ni kupunguza ajali hizi kote nchini”alisema Kahatano.

Hata hivyo alikiri kuelemewa na utekelezaji wa jukumu la kukamata waendesha pikipiki  wanaovunja sheria barabarani kutokana na wingi wao ukilinganisha na uchache wa Askari wa usalama barabarani.
Kwa sasa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Sumatra limeingia makubaliano na halmashauri zote nchini kuanzia Julai mwaka huu kutoa leseni ya biashara kwa kila dereva wa bodaboda ili kuwatambua rasmi na kupunguza matukio ya ukabaji dhidi yao.

Aidha aliwataka madereva wote na wamiliki wao kutambua sheria za barabarani na kujali uhai wao pindi wanapokuwa barabarani  na kwamba endapo kila mmoja atafanya hivyo itakuwa ni njia sahihi ya kupunguza au kumalizika ajali hizo.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate