Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Prof.
Costa Mahalu ameshinda kesi ya ubadhirifu wa mali ya umma na kuiingizia
hasara Serikali, iliyokuwa ikimkabili kwa miaka saba katika Mahakamu ya
Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam.
Prof. Mahalu ambaye alikuwa mshitakiwa namba moja kwenye kesi ya matumizi mabaya ya fedha za ununuzi wa jengo la ubalozi wa Tanzania nchini Italia, pamoja na mshitakiwa namba mbili Grace Martin walishinda kesi hiyo kwa hakimu kusema washitakiwa hawakuonekana na hatia yoyote kutokana na kukosekana kwa ushahidi uliokamilika kwa kila shitaka.
Hukumu hiyo iliyoanzwa kusomwa kuanzia saa sita mchana na Hakimu Mfawidhi Ilvin Mgeta ambaye ndiye alikuwa akisikiliza kesi hiyo, ilidumu kwa muda wa saa moja u nusu.

Prof. Mahalu akizungumza na wanahabari
Prof.
Mahalu na Grace Martin (kushoto) wakiwa wamezungukwa na Waandishi wa
Habari muda mfupi baada ya kusomewa hukumu ya kesi yao ambayo wameshinda
(picha via Michuzi Blog)
Grace Martin (katikati), akisaidiwa na ndugu zake kutoka Mahakamani (picha: Richard Mwakienda "Kamanda wa Matukio")
No comments:
Post a Comment