MKUU
wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu ameonya walimu wa shule za msingi
sekondari na vyuo mkoani hapa kusitisha mara moja mgomo na badala yake
warudi kuendelea kufundisha hasa ikizingatiwa kuwa wanafunzi wa shule
za msingi na sekondari wanajiandaa kuanza kufanya mithiani yao hivi
karibuni.
Wito huo ameutoa jana wakati aakizungumza na walimu wakuu wa shule zote za halmashauri ya Manispaa ya songea kwenye
ukumbi wa chuo kikuu huria mjini Songea,amesema kila mwalimu anapaswa
kutambua umuhimu alionao katika jamii hivyo ni vema kuachana na
vishawishi vya kuendeleza migomo ambao unatolewa na chama cha walimu.
Mwambungu
ameongeza kuwa,kwanzia sasa mwalimu yoyote ambaye hataonekana
kuhamasisha mgomo kwa walimu wenzake atachukuliwa hatua kali za
kisheria kwani mgomo huo siyo halali na tayari serikali imeshapeleka
swala hilo mahakamani kwa ajili ya usuluhishi.
Amefafanua
zaidi kuwa kila mwalimu kwanzia sasa hahakikishe kuwa anakuwepo katika
eneo lake la kazi na anaingia darasani kufundisha na sio kwenda
kusaini na kutoka kwani watakuwa wanapita na kuandika majina ya walimu
ambao wamehudhuria kazini na kufundisha.
“Naomba
muwaambie walimu wote warudi shuleni kufundisha kwani kila kila mtu
aliomba kazi peke yake ,na ambao watakahidi agizo hili watachukuliwa
hatua za kisheria,na hatuta mvumilia kiongozi yoyote ambaye ataonekana
amehamasisha mgomo huo,”alisema Mwambungu.
Aidha,amewashauri walimu hao kuwa wavumilivu wakati serikali inashugulikia madai yao , nao wawape haki ya msingi wanafunzi hao.
Kwa upande wake katibu
wa chama cha walimu mkoa wa Ruvuma Luya Ngonyani amesema mgomo huo ni
halali na upo palepale kwani umezingatia sheria ya ajira na mahusiano
kazini hivyo hali halisi ya mgomo mkoani Ruvuma umeitikiwa kwa shule nyingi za msingi, sekondari na chuo cha ualimu cha Songea.
Ngonyani
ameongeza zaidi kuwa ni walimu wachache ambao wameonyesha
kutokukubaliana na mgomo huo lakini bado wanaendelea ili kuwashawishi
waungane na walimu wenzao ili kuhakikisha kuwa mgomo huo unakwenda kama
CWT ilivyotaka.
Wakati
huohuo baadhi ya shule za msingi zikiwemo Matalawe, mfaranyaki, maji
maji na misufini zimewarudisha wanafunzi majumbani na kuwataka kurejea
shuleni hapo siku ya ijumaa ambayo shule zote zitafungwa rasmi.
No comments:
Post a Comment