Rais wa Misri , Mohammed
Mursi, ameahidi kuwa vikosi vya usalama vya Misri, vitachukua uthibiti
kamili wa rasi ya Sinai baada ya shambulio lililotokea kwenye mpaka
baina ya nchi hiyo na Israel.
Watu waliojihami kwa silaha waliwauwa walinzi sita wa mpaka wa Misri.
Israel
ilisema washambuliaji waliokuwa wamejihami kwa silaha nzito walichukua
magari ya kijeshi na kujaribu kulazimisha kuvuika mpaka huo .
Shambulio hilo lilitokea jioni katika kizuizi
cha mpakani wakati wanajeshi walikuwa wakifunga kazi tayari kwa futari
wakati huu wa mfungo wa mwezi wa Ramadhan.
Televisheni inayomilikiwa na serikali nchini
Misri imesema kuwa kundi la watu waliojihami kwa mbuduki na maguruneti
ya kurushwa kwa roketi liliwashambulia wanajeshi hao kabla ya kutoweka
na gari moja la kivita.
Msemaji wa jeshi la Israel, hata hivyo alisema
magari mawili yalitekwa na kwamba moja lililipuka karibu na eneo la
kivuko cha mpakani la Kerem.
Gari la pili lililengwa na jeshi la wanahewa la Israel.
Tukio hilo litachukuliwa kama ushahidi wa kutia
wasiwasi kwamba wanamgambo wa Kiislamu wanathibiti eneo la kaskazini mwa
Jangwa la Sinai.
Wanamgambo hao wamelaumiwa kurusha maroketi kadhaa nchini Israel na kuwauwa Waisraeli tisa mwaka uliopita.
Wakati hali ya wasiwasi ikizidi kutanda Misri
imetuma vifaru zaidi na wanajeshi katika eneo la Sinai-Mpango huo
ulitekelezwa kwa makubaliano na Israel katika mkataba wa amani wa mwaka
1979.
Israel imeitaka Misri kuchukuwa uamuzi wa mara moja.
Tukio hilo limejiri wakati Israel ikitangaza
kuwa inaboresha makombora yake ya masafa marefu aina ya Ballistic
kukabiliana na kile inachokiona kuwa tishio la usalama wake linalozidi
kujitokeza katika eneo la
Mashariki ya Kati.
Mradi huo wa kujenga makombora ya masafa marefu unatekelezwa na serikali ya Israel kwa ushirikiano na Marekani.
Hii ni baada ya Iran kutangaza kuwa imefanikiwa
katika kufanyia majaribio makombora yake ya masafa mafupi aina ya
Ballistic, yaliyoboreshwa zaidi.
No comments:
Post a Comment