Natasha Mwigizaji mwandishi wa muswada Swahiliwood. |
“Tasnia ya filamu hailipi kabisa, kuna wakati ambao unaona kabisa
jinsi ukipoteza muda wako katika kuhangaika na jambo lisilo lipa wakati
kwa wenzetu ni ajira rasmi, unatumia nguvu kubwa lakini linavyokuja
suala la malipo au kuuza filamu husika unababaishwa na wanunuzi jambo
linatengeneza mazingira ya wasanii kujikuta wakidhulumiana kutokana na
mazingira yaliyopo,”anasema.
Natasha anasema kuwa anatumia muda mwingi katika kuchagua filamu za
kushiriki ikiwa katika kuwaunga mkono wasanii wachanga lakini si katika
kutengeneza fedha, huku akisema kuwa mara nyingi katika tasnia ya filamu
kumekuwa na taarifa zisozo sahihi kutoka kwa baadhi ya wasanii ambao
wamekuwa wakijinadi kuwa wanalipwa fedha nyingi kwa kushiriki filamu
hizo.
Natasha akiwa na pacha wake Monalisa ambaye ni mwanaye. |
“Kuna wakati ambao baadhi ya wasanii wamekuwa wakidanya kama wanalipwa
fedha kuanzia milioni kwenda mbele jambo hili si kweli, mfano filamu
inawashiriki zaidi ya 20 kila msanii akilipwa milioni tu, ukichanganya
na gharama za uandaaji filamu hiyo gharama zake zinaweza kufikia hata
milioni 25, je ni filamu ngapi ambazo zinauzwa zaidi ya milioni 35? Hapo
ndio utabaini ukweli,”anasema Natasha.
No comments:
Post a Comment