EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, August 9, 2012

Tamko la Prof. Shivji kuhusu habari ya "Shivji, Lwaitama wataka Muungano uvunjwe"

JUU YA MUUNGANO: TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 


Nimeshitushwa na gazeti moja la kila siku  (Tanzania Daima la tarehe7 Agosti 2012) lilonipandikizia maneno katika kichwa chake cha habari kwamba ‘Shivji, Lwaitama wataka Muungano uvunjwe’. Siwezi nikamsemea Dr. Lwaitama lakini kwa upande wangu sijasema wala kumaanisha kwamba ‘Muungano uvunjwe’.

Nikitoa mchango wangu baada ya mada mbili kuwasilishwa na Prof. Abdul Sheriff na  Dr. Azaveli Lwaitama, nilisisitiza mambo haya matatu ya msingi.

Mosi, kwamba wasomi, wakiwemo wanahabari, wana jukumu zito la kutokupinda  ukweli wa kihistoria kwa lengo la kuhalalisha mtazamo na msimamo wao kuhusu  Muungano. Nikatoa mfano wa jinsi Merehemu Sheikh Karume anavyodekezwa  katika msimamo wake juu ya Muungano. Wasemaji hapa bara wanamsifu kwa kuwa  muasisi mwaminifu na mshabiki mkubwa wa Muungano tangu mwanzo. Huko  Zanzibar, wasemaji hawachoki kumnukuu Mzee Karume kuwa tangu mwanzo yeye  hakutaka Muungano isipokuwa alikuwa anafikiria Shirikisho.

Wanaendelea kusema kwamba aliposaini Mkataba wa Muungano, Mzee Karume alifikiri kwamba anasaini Shirikisho la Serikali tatu, lakini kutokana na kiwango cha  elimu yake hakuelewa vizuri mantiki na maana ya alichokuwa anasaini.

Nikaendelea kueleza kwamba maelezo haya yote mawili hayaungwi mkono na ushahidi wa kihistoria. Ukweli ni kwamba, Mzee Karume aliingia katika Muungano kutokana na hesabu zake mwenyewe za kisiasa. Muungano kwake ulikuwa njia ya kuondoa upinzani, au upinzani tarajiwa, wa utawala wake. Yaani ilikuwa ni tendo la mwanasiasa yeyote yule kudumisha utawala wake (political survival).

Na kwa watawala wote wa Zanzibar waliomfuata, wakiwemo wa upinzani, ndivyo ilivyokuwa. Wamekuwa wakitumia mwavuli wa muungano wakati utawala wao uko hatarini na kushawishi wananchi wao dhidi ya muungano wakitafuta umaarufu wa kisiasa.

Nikitoa mfano nikasema kwamba kuna taarifa kwamba chama kimoja huko Zanzibar kinapandikiza pendekezo la ‘muungano wa mkataba, sio wa katiba’ bila ya kueleza waziwazi maana yake. Ukweli ni kwamba huwezi ukawa na muungano wa mkataba bila kwanza kuuvunja muungano. Kwa hivyo, wanachoshawishi moja kwa moja ni kuuvunja muungano. Basi waseme hivyo badala ya kujificha nyuma ya pazia la ‘muungano wa mkataba’.

Jambo la pili nililorudia ni kwamba tuliangalie suala zima la muungano kwa mtazamo na maslahi na matakwa ya Umma wa Zanzibar na Umma wa Tanzania bara, hususan matabaka ya hali ya chini. Katika hali yao kimaisha – kiuchumi na kisiasa – hakuna tofauti kati ya wananchi wa Zanzibar na wananchi wa Tanzania bara. Uduni wa hali yao ni uleule; ukosefu wa ajira ni uleule; kutokuwa na mfumo wa dhati wa demokrasia unaojali walalahoi ni kulekule.

Kwa hivyo, umuhimu kwao ni mshikamano wao kuboresha mifumo ya uchumi na siasa. Wasiburuzwe na wanasiasa na vyama vyao kwa maslahi yao binafsi ya muda  mfupi ya kudumisha, au kuingia kwenye, utawala.

Jambo la mwisho nililogusia ni kwamba kiini cha suala la muungano si idadi ya serikali (mbili au tatu) bali ni mgawanyo wa madaraka (distribution of power) kati ya  dola la Zanzibar na dola la Muungano. Na katika hili kila muungano duniani ni wa kipekee kutokana na hali halisi yao ya kihistoria na uwiano wa kisiasa. Sisi pia tukiwashirikisha wananchi kikamilifu na tukaelewa vizuri matakwa yao tunaweza kubuni muundo wetu wa muungao ambao ni wa kipekee bila kujali idadi ya serikali.

Nimeona niweke wazi mtazamo wangu kwa sababu ya baadhi ya vyombo vya habari kuwa na hulka ya kupotosha mambo kutokana na ushabiki wao bila kujali madhara  yanayoweza kutokea.

Mwishoni ningependa kusema kwa dhati kwamba uvunjaji wa muungano hauwezi kuwa kwa manufaa ya walio wengi. Ukweli ni kwamba unaweza ukasambaratisha  nchi na jamii zetu pande zote mbili za muungano. Tukianza kubaguana kati ya Watanganyika na Wazanzibari, tutaendelea kubaguana kwa msingi wa Uislamu na  Ukristo, na Usukuma na Uchaga, Uarabu na Uafrika, weusi na weupe bila kikomo.

Kama alivyosema Mwalimu, ukishaonja nyama ya mtu basi utaendelea kumtafuna.

Issa Shivji
Profesa wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere,
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Agosti 8, 2012

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate