Tukio hilo lilifanyika muda mfupi kabla ya treni iliyombeba Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe haijafika katika kituo hicho.
Msafara wa Dk. Mwakyembe aliyeambatana na waandishi wa habari pamoja na maofisa wa Sumatra na wale wa Shirika la usafirishaji la Tanzania na Zambia (TAZARA), ulikuwa unarejea stesheni ya Dar es Salaam, ukitokea katika kituo cha Mwakanga nje ya jiji.
Safari hiyo ilikuwa ni baada ya Waziri Mwakyembe kuzindua usafiri wa aina hiyo kwa treni ya Shirikla la Reli nchini (TRL), uliofanyika eneo la Ubungo Maziwa.
Mmoja wa maofisa wanaolinda katika eneo hilo la Yombo, aliyeomba jina lake lihifadhiwe kwa kuwa si msemaji, alisema kuwa walimkamata kibaka huyo wakati akitekeleza uhalifu wake pasipo kuhofia athari zitakazojitokeza endapo behewa hilo lingeanza kufanya safari zake.
Kufuatia tukio hilo kibaka huyo alibebwa katika moja ya mabehewa yaliyombeba Waziri Mwakyembe na kisha kufikishwa katika Kituo cha Polisi Tazara kwa hatua zaidi.
Awali, Waziri Mwakyembe akizindua treni hizo za Tazara na TRL kwa ajili ya usafiri wa ndani ya Jiji la Dar es Salaam, akisema amefurahishwa kuona ndoto yake imetimia na kutoa pongezi kwa mafundi wa mashirika hayo kusiamama kidete kuhakikisha usafiri huo unaanza kama walivyopanga.
Dk. Mwakyembe alisema usafiri huo ulikuwa ukisubiriwa kwa muda mrefu na wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, hivyo kuwataka kuhakikisha kuwa wanatunza miundombinu iliyopo kwa ajili ya kuokoa fedha za Watanzania zilizotumika kuboresha hali hiyo.
“Kumbukeni kulikuwa na changamoto nyingi juu ya huu mradi, kipekee niwashukuru mafundi wa mashirika yote mawili waliowezesha kufanyika kwa haya mnayoyaona leo, kwa maana waliponiambia inawezekana, mwanzo niliitikia nikiwa siamini kama muda huu watakuwa wamekamilisha kazi, kwa namna mabehewa yalivyokuwa yamechakaa,” alisema.
Aliongeza kuwa kama serikali itaamua kuwekeza kwa dhati kwa Watanzania basi wanaweza kufanya mambo makubwa kwa muda mfupi kama ambavyo imedhihirishwa katika harakati za kuwapatia usafiri wa treni katika Jiji la Dar es Salaam.
Naye Naibu Mkurugenzi wa Tazara, Damas Ndumbaro, alisema wamejipanga kutoa huduma bora ya usafiri ikiwa ni pamoja na kudhibiti mapato yatokanayo na uuzwaji wa tiketi za kila siku.
Habari na Abdallah Khamis.
No comments:
Post a Comment