MWIMBAJI
nyota wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini, Adelina Sanga (Linah),
amesema mikakati yake ni kuhakikisha kuwa anaendelea kutamba ndani na
nje ya nchi kwa kufanya makubwa kwenye tasnia hiyo na kamwe hatabweteka
kwa mafanikio machache aliyoyapata hadi hivi sasa.

Msanii huyo aliyetokea katika nyumba ya kukuza na kulea vipaji,
Tanzania House of Talents (THT), sasa anafanya kazi kwa kujitegemea
mwenyewe baada ya kufanikiwa kuonyesha uwezo wake katika muziki wa Bongo
Fleva.
Linah alisema kwamba mikakati hiyo itamuwezesha pia kuwika kimataifa,
kama alivyozea kupata shoo katika nchi mbalimbali, ikiwamo Uingereza
anayokwenda kila wakati.
Alisema kwamba sanaa yake inatokana na mipango yake pamoja na ujuzi wa
kuimba kwa ajili ya kuwapatia burudani kamili mashabiki wake waliozagaa
katika mikoa mbalimbali na kupenda nyimbo na shoo zake.
“Nafanya mikakati kwa ajili ya kuendelea kuwa juu katika ramani ya
muziki wa kizazi kipya kwa kutoa nyimbo nzuri au kutoa burudani kwa
kuangalia mashabiki wangu wanahitaji nini kutoka kwangu kwa ajili ya
kuwa nao sawa” alisema Linah.Via saluti5.
No comments:
Post a Comment