MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi
Kavu na Majini (Sumatra), itasitisha utoaji wa leseni mpya za
usafirishaji wa abiria katika Jiji la Dar es Salaam kwa mmiliki mmoja
mmoja kuanzia Desemba Mosi mwaka huu.
Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi Mkuu wa
Sumatra, Ahmad Kilima, ilisema hatua hiyo inatokana na kushauriana kati
ya Sumatra, wamiliki wa Daladala, Mradi wa Mabasi yaendayo Kasi (Dart)
na wadau wengine.
Baadhi ya wamiliki waliomba kuwepo kwa elimu ya kutosha kwa wamiliki juu ya mfumo huo mpya kabla ya kuanza kuutekeleza.
Katika taarifa yake, Kilima alisema safari ambazo
zitasitishiwa utoaji wa leseni ni za Barabara ya Kilwa kuanzia Mbagala
kwenda katikati ya Jiji na maeneo mengine.
Barabara nyingine ni ile ya Ali Hasani Mwinyi kuanzia Mwenge kwenda maeneo ya katikati ya jiji.
“Kuanzia Juni 30, mwaka kesho, mamlaka itasitisha
uendeshaji wa leseni kwa mmiliki mmoja mmoja anayetoa huduma katika
barabara zilitotajwa” alisema Kilima.
Alisema kwa wale ambao leseni zao zinaisha kabla ya Juni 30 mwaka kesho, mamlaka itaendeleza leseni zao kwa kuwapa leseni za muda mfupi zinazoishia Juni 30 mwakani.
“Katika kipindi cha kuanzia Desemba mosi mwaka huu
hadi Juni 30 mwaka kesho, wasafirishaji wanaotoa huduma katika njia
hizo, wanashauriwa kujiunga na kuanzisha makampuni au ushirika ili
waweze kupewa leseni za kutoa huduma kuanzia Julai Mosi mwaka kesho,”
alisema.
Alisema vigezo na masharti ya leseni za usafirishaji yatazingatiwa katika utoaji wa leseni hizo mpya.
Katika mkutano huo, Sumatra ilisema hali ya utoaji
huduma katika jiji hairidhishi kutokana na kutokuwepo kwa utaratibu wa
wamiliki kuwasimamia madereva na makondakta.
No comments:
Post a Comment