KUFUATIA mkutano ulioitishwa na baadhi wa wanachama wa Simba Jumapili hii, Baraza la Wazee wa klabu hiyo ya mtaa wa Msimbazi, limewataka wanachama hao kutoitisha mkutano huo kwa vile mkutano huo si halali.
Kaimu
Katibu Mkuu wa Baraza hilo, Zuberi Mpacha, alisema jana kuwa si kweli
kuwa wanachama wakifika 500 wanakuwa na uwezo wa kuitisha mkutano.
Zuberi alisema kuwa mkutano bila ya ridhaa ya uongozi si halali hivyo kufanya hivi itakuwa kinyume na katiba ya Simba.
Akinukuu
baadhi ya vifungu vya katiba ya Simba, Zuberi alisema kifungu cha 22
kinakataza kuwepo kwa mkutano bila ya ridhaa ya viongozi.“Baraza la
Wazee tunasema mkutano huo si
halali kabisa, kama kuna matatizo ndani ya uongozi kuna sehemu ya
kusuluhisha na si kutumia mikutano ambayo si halali” alisema Mpacha.
Baadhi
ya wanachama wameitisha mkutano wa dharura kupinga uongozi wa klabu
kufutia kufanya vibaya katika mzunguko wa kwanza wa Ligi kuu Tanzania
Bara.Via saluti5.
No comments:
Post a Comment