KUDAMKA KUPIGA DEKI KWENYE KORIDO WAKATI KUNA
WAGENI WAMELALA
NI jambo la ajabu sana, utakuta mwanamke amepata
wageni, ndugu wa mumewe wametokea kijijini. Kwa sababu sehemu ya kulala ni
finyu, mume anamwambia mkewe watandikiwe kwenye korido ndani walale maana
watakaa siku mbili au tatu tu.
Cha ajabu sasa, mke huyo anayeonekana ana busara
zake, anadamka saa kumi na moja alfajiri na kuanza kupiga deki hivyo kuwafanya
wageni waamke na kwenda kukaa nje kwa sababu ya maji, tena ya baridi maana ni
asubuhi. INAKERA SANA.
HII NAYO INAKERA
MKE KUULIZWA CHUMBANI, KWENDA KUJIBA SEBULENI
UTAKUTA mke wa mtu yuko na mumewe chmumbani,
anamuuliza ‘dear ni kwanini leo chakula kinanuka sana moshi?’ mke badala ya
kujibu kulekule chumbani, anatoka kama vile hajamsikia mumewe, akifika sebuleni
ndiyo anaanza:
“Si ungepika wewe kama unajua kupika. Moshi moshi,
wenzako Somalia wanatafuta chakula hata kinachonuka kinyesi hawakipati, acha
hizo.”
Inakera sana, ukizingatia sebuleni anakokwenda
kujibia kumepakana na dirisha la nyumba nyingine ya pili!
INAKERA SANA
SANA
MGONJWA YU
HOI, MHUDUMU MAPOKEZI HANA HILI WALA LILE
Hata Mungu
hapendi! Kwamba, mtu anaumwa, ugonjwa wowote ule, hali inakuwa mbaya sana,
nduguze wanamkimbiza hospitali.
Kufika
mapokezi, mhudumu anaendelea na mambo mengine bila kujali, anatokea mlinzi na
kumwonesha ndugu wa mgonjwa mahali pa kuchukua ‘wheel chair’ kwa ajili ya
kumbebea mgonjwa wake ambaye amelala kwenye ngazi na kumpeleka kwa daktari.
Hii ilitokea
hivi karibuni katika hospitali moja ya wilaya ambapo mlinzi aliyemwonesha wheel chair ndugu wa mgonjwa, alikiri
tabia hiyo kuota mizizi mahali hapo. Inakera sana!
INGEKUWA VIPI?
INAKERA SANA
WAHUDUMU BAA KUTOKA
CHOONI BILA KUNAWA KWA SABUNI
NI jambo ambalo lipo
sana, utawaona baadhi ya wahudumu wa baa ‘mabaamedi’ wanaingia chooni na kukaa
kwa karibu dakika tano kuashiria kuwa wako kwenye kushusha ‘mzigo mkubwa’,
lakini cha ajabu wakitoka hapo hawaonekani kunawa mikono kwa maji na sabuni
kama inavyoelekezwa na afya ya jamii.
Mbaya zaidi,
wanaendelea kuhudumua wateja, pengine kwa kuwapelekea kongoro, mchemsho au
kushika glasi ya kunywea kinywaji. Hii INAKERA SANA!
-----------------------------------------------------------------------------------------------------VYOO VYA HOSPITALI VIKIWA VICHAFU, VYA MTAANI VITAKUWAJE?
Inasumbua sana akili kukuta vyoo vya hospitali eti ndiyo vichafu, havitazamiki, havina maji, uchafu nnjenje, je vya uswahilini vitakuwaje?
Utafiti uliofanywa katika baadhi ya hospitali, tena zaidi sana zile za serikali umebainisha kuwa licha ya kuwepo kwa wahudumu kwenye vyoo hivyo, lakini hakuna cha maana kinachofanyika ili kuvifanya viwe visafi.
Kwa mujibu wa mgonjwa mmoja aliyelazwa kwenye hospitali moja ya serikalk iliyopo wilayani Kinondoni, Dar, wahudumu wanaoshughulikia usafi kwenye vyoo hivyo wanapokumbushwa na wagonjwa kuhusu usafi au kuwepo kwa maji huonesha dalili za kukereka kwa kuambiwa huko.
Mbaya zaidi, mganga mkuu wa hospitali hiyo anajua malalamiko ya kuwepo kwa vyoo vichafu, lakini hachukui hatua yoyote na anaendelea kuidhinisha mishahara ya watumishi hao kila mwezi.
Hii ni kero sana tunaomba wahusika mjirekebishe!
---------------------------------------------------------------------------------------------------
WANA NINI HAWA MADEREVA WANAOONGEZA FOLENI KWENYE BARABARA MOJA?
Ziko barabara za njia
mbili “Two Way”, lakini pia ziko za “One Way”. Mfano barabara ya kutoka
Shekilango kwenda Mwenge ni “One Way”. Ina maanisha kwamba gari likiwa
limesimama mbele barabarani, dereva wa nyuma hawezi kupita kama mbele kutakuwa
na gari linalokuja.
Utakuta magari yapo Sinza
Kijiweni foleni ni kubwa sana. Daladala zinakuja kutoka Shekilango na kukuta
foleni hiyo. Cha ajabu sana sasa, madereva wa hizi daladala anakuja na kuyapita
magari mengine ya mbele yake kwa kuingia njia ya pili ili awahi.
Kinachotokea hapo ni
kukutana uso kwa uso na magari yanayotoka Sinza Kumekucha ambayo nayo
yatashindwa kwenda mbele kwa sababu ya kuzuiwa na hao madereva vichwa ngumu
wasiojua sheria waliokuwa wakitokea Shekilango na hivyo kuifanya foleni kuwa
kubwa sana.
Askari wa Usalama
Barabarani wangeliangalia hili ikiwezekana kutoa adhabu kali ili hawa wajinga wanaosababisha
foleni bila msababu wajifunze.
------------------------------------------------------------------------------------------------------------Jamani wengi wetu wanaamini biashara asubuhi jioni ni mahesabu si ndio ee? Unashangaa nini kwani wewe haujawahi sikia kauli hiyo? Usizuge bhana hilo lako na kama si lako basi ni la jirani yako.
Eeh kuna watu
wanajifanya akili zao hazina kitu kabsaa sijui wamerogwa! Eti utawakuta
asubuhi na mapema muda wa wenzao kufanya biashara wao wanaleta kujuana,
me wananikera vibaya mno! Mapema hata chai hawajanywa utawakuta hao
wanakwenda kwenye vibanda vya wauza magazeti kwenda kusoma magazeti!
Makubwa ya jongo! Yaani mwenzio yupo kwenye biashara we unakwenda kuleta
Ujinga wako jamani! Kwani uliambiwa yeye anatoa msaada wa magazeti ya
bure! Hata haya huna unakwenda kumzingira kijana wa watu anapojitafutia
riziki hii halali kweli? Tena utakuta wamerundikana rundo utadhani
wananunua? Mna akili kweli nyie! Inafikia hatua mnunuzi akija anashindwa
hata
kununua kwa jinsi mlivyorundikana utadhani pamechinjwa mtu!
kununua kwa jinsi mlivyorundikana utadhani pamechinjwa mtu!
Mnanikera mbayaa! Na kama kila mtu atatoka ntumbani kwake na kwenda kusomea hapo kibandani huyo muuzaji atapata riziki yake kweli! Na ile kauli ya biashara asubuhi jioni mahesabu italeta maana kweli! Maana jioni hatokuwa na mahesabu! Ahesabu nini wakati wanunuzi mmejisomea palepale tena kitu free bila ushuru wala bhugudha! Na hao wanaozalisha hayo magazeti si ndio maana wengi biashara inawashinda!
Wasifunge mchezo,
wabongo wanapenda free utadhani maiti kha! Ebu kuweni wastaarabu bhana
fanya kazi upate ela yako ununue gazeti usome kwa raha zako! Najua hapo
mmenuna si limewagusa teh teh mtalinywa tu hata kama chungu si ndiyo
dawa jamani! Haya nisameheni lakini meseji send kama hautaki we mbishi!
Km hautaki kadeki bahari ciao
No comments:
Post a Comment