Vinara wa ligi kuu ya Premier ya England kwa sasa
Manchester United inajiandaa kuendelea uongozi wao wakati watakapoialika
Newcastle siku ya leo.
Mabingwa watetezi Manchester City nao watakuwa nyumbani kucheza na Sunderland.
Katika
mechi zingine, Reading inayoshikilia nafasi ya mkia imepangiwa kucheza
na Swansea, West Brom nayo kusafiri ugenini kupepetana na QPR.
Baada ya kuandikisha matokeo yasiyoridhisha
katika mechi yao ya mwishoni mwa juma lililopita, Manchester United
itakuwa ikipania kujiimarisha kileleni mwa ligi hiyo kwa kuandikisha
ushindi.United ilitoka sare mechi yao ya mwisho dhidi ya
Swansea na kufikia wakati huu bado imo alama nne tu mbale ya mabingwa
hao watetezi.
Vilabu hivyo viwili vilipoteza mechi zao za
tarehe 26 Desemba msimu uliopita uliopita na makocha Alex Ferguson na
Roberto Mancini tayari wametoa onyo kwa wachezaji wao kuzuia matokeo
kama hayo.
Baada ya kuandikisha ushindi wa magoli manane kwa yai dhidi ya Aston Villa, Chelsea imeratibiwa kucheza na Norwich.
Liverpool kutoana jasho na Stoke city na Fulham kualika Southampton katika uwanja wao wa nyumbani wa Craven Cottage.
Mechi kati ya Arsenal na West Ham imehairishwa kutokana na uwezekano wa kuwepo kwa mgomo wa madereva wa treni.
Totten kuchuana na Aston Villa na Everton kucheza dhidi Ya Wigan.
No comments:
Post a Comment