KWA
wapenzi wa Manchester United hali ilikuwa ni ya kihoro katika mchezo wa
Ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Newcastle uliochezwa kwenye uwanja wa
Old Trafford.
Manchester
United ililazimika kusawazisha mara 3 na hatimaye kupata bao la nne
dakika ya tisini lililoipa ushindi wa mbinde wa 4-3.
Hernendes akipiga bao la nne na la ushindi
Imekuwa
ni kama jadi sasa kwa United kutoka nyuma na kuibuka na ushindi, hali
ambayo imekuwa ikiwaweka roho juu mashabiki wake katika kila mchezo.
Newcastle walianza kuongoza dakika ya 4 ya mchezo kwa goli la James Perch, John Evans akasawazisha dakika ya 25.
Newcastle wanaadika bao la kwanza
John Evans anaiswazishia Manchester United
Dakika
tatu baadae, juhudi za Evans zikawa ni kama kazi bure, dakika 28 akaipa
Newcastle bao la zawadi pale alipojifunga katika juhudi zake za kuokoa,
goli ambalo lilizua utata mkubwa miongoni mwa waamuzi.
Evans anajifunga, bao la pili kwa Newcastle
Mshika kibendera anasema sio goli
Refarii anasema ni goli, Newcastle wanashangilia 2-1
Kipindi
cha pili dakika ya 58 Evra akaisawazishia Manchester United, lakini
Newcaslte wakawa mbele tena dakika ya 68 kwa bao safi la Cisse.
Robin
Van Persie akairudisha mchezoni Manchester United kwa goli la dakika ya
71, hili likiwa ni goli lake la 13 kwa United katika Ligi kuu ya
Uingereza tangu alipojiunga nayo mwanzoni mwa msimu huu.
Shujaa
wa mchezo akawa ni Javier Hernandes pale alipoitumia vema pasi ya
kiungo Michael Carrick na kufunga bao maridadi dakika ya 9o.
Katika mchezo mwingine, Liverpool ilichapwa na Stoke City 3-1, huku Totenham Spurs ikivuna ushindi wa 4-0 kwa Aston Villa.
Matokeo ya mechi zote zilizochezwa jana ni kama ifuatavyo:
Everton 2 – 1 Wigan
Fulham 1 – 1 Southampton
Manchester United 4 – 3 Newcastle United
Norwich 0 – 1 Chelsea
Reading 0 – 0 Swansea
Sunderland 1 - 0 Manchester City
Queens Park Rangers 1 – 2 West Bromwich Albion
Aston Villa 0 – 4 Tottenham
Stoke City 3 – 1 Liverpool
No comments:
Post a Comment