JUMUIYA ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)
wilayani Kahama, umedhamiria kufanya maandamano ili kushinikiza
kuwang’oa watumishi wa serikalini waliopo ndani ya wilaya hiyo ambao
utendaji kazi wao umekuwa kero kwa jamii.
Akizungumza na waandishi wa habari jana wilayani hapa, Mwenyekiti wa
umoja huo, Solomoni Mataba, alisema wamedhamiria kuwang’oa katika nafasi
zao watumishi wasio waadilifu, wanaochangia kuipaka matope serikali
iliyopo madarakani.
Alisema kuwa wamejipanga kuwafichua wasiofuata maadili ya uwajibikaji
kazini na kuwa kero, ikibidi kwa kufanya maandamano ili wakazi wa wilaya
hiyo waweze kupata haki yao.
Mataba aliwataka watumishi waliosahau wajibu wao huku wakijifanya
miungu watu, kuhakikisha wanafuata maadili na kuacha kufuata maslai
binafsi ambayo imekuwa sababu kubwa ya jamii kuichukia serikali.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa baadhi ya idara zimejisahau, huku
zikiwanyanyasa wananchi hatua ambayo inazidisha chuki kwa serikali yao.
No comments:
Post a Comment